Chama cha Mrema TLP Chataka Zanzibar Imtenge Maalim Seif

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

CHAMA cha Tanzania Labour(TLP) kimemuandikia barua Rais wa Mapinduzi wa Zanzibar, Dk Mohamed Ali Shein na kumtaka kuanzia sasa wamtenge Katibu Mkuu wa CUF , Maalim Seif Sharif Hamad (pichani), kwa kutomualika kwenye shughuli zozote za kitaifa mpaka atakapojirekebisha na kuitambua rasmi serikali iliyopo madarakani.

Aidha, kwa kuwa CUF inadai kwamba haiitambui serikali hiyo basi ruzuku kwa chama hicho isitishwe kuanzia sasa hadi hapo chama hicho kitakapoitambua rasmi serikali hiyo na kuacha kuhamasisha wananchi wasilipe kodi.

Katika barua ya chama hicho iliyosainiwa na Mwenyekiti wake, Augustine Mrema ilisema chama hicho kimesikitishwa na wanalaani kitendo kilichofanywa Hamad ambaye pia alikuwa Makamu wa kwanza wa Rais kwenye serikali ya Umoja wa kitaifa wa Zanzibar (SUK) wakati wa maziko ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa serikali ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar, marehemu Mzee Aboud Jumbe cha kukataa kumpa Rais Shein mkono wa kusalimiana.

Alisema kuleta tofauti za kisiasa msibani kwa makusudi, Maalim Seif ameendelea kuwagawa Wazanzibari kisiasa na kushindwa kumuenzi marehemu Aboud Jumbe, ambaye pamoja na kuiongoza Zanzibar kwa amani na utulivu pia ndiye aliyemlea Maalim Seif kisiasa.

Alisema tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa marudio uliosusiwa na CUF, Maalim Seif amekuwa akileta chokochoko na uchochezi dhidi ya serikali ya Zanzibar akidai kwamba haitambui na kuwataka wananchi wa Zanzibar kugoma na kuwataka wasilipe kodi kwa serikali
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hapo kuna ukweli kidogo japo ni kama unatetea kitu fulani upange wa Shein.Kwa kiongozi kuonyesha tabia ya kisasi sio jambo jema,
    Alikataa hata kusalimiana na Lipumba,hafai Cuf wanapashwa kuangalia hilo.

    ReplyDelete
  2. anasema nini mrema maiti jeuri na kushughulikia yasiyokuhusu, maalim sio saiz yako

    ReplyDelete

Top Post Ad