Godbless Lema Afungukia Mauaji ya Askari Wanne Dar, Adai ni Ishara Mbaya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kwanza ninawapa pole familia za Polisi wote waliouwawa waliokuwa kwenye majukumu yao ya ulinzi wa raia na mali zao.

Ni huzuni kubwa Polisi kuuwawa na silaha kwenda kwenye mikono ya wahalifu, tukio kama hili ni muhimu likatukumbusha kwamba Taifa linaweza kujengwa vyema kama kila mmoja atawajibika katika haki na sheria , kumbe Polisi wanaweza kuuwawa na Watu wasio na huruma na wasiotii sheria , kama ambavyo Polisi wasio na huruma na utii kwa Katiba wanavyoweza kujiandaa kuvunja ukuta unaotaka uwajibikaji wa matumizi sahihi ya Katiba na sheria.

Ni ishara mbaya sana kuona walinzi wetu wanauwawa, lakini ni ishara mbaya zaidi kuona walinzi wetu wakiwa kwenye mazoezi hadharani ya kujipanga kudhibiti na pengine hata kuua Wananchi wanaodai haki yao Kikatiba ya mikutano ya vyama vya Siasa.

Uimara wa Jeshi letu utajengwa na uhusiano mzuri kati yake na raia na sio silaha za kisasa na mazoezi ya vitisho hadharani.

Poleni sana Watanzania kwa tukio hili baya, ni matumaini yangu kuwa watu hawa watatiwa nguvuni haraka iwezekanavyo.

Godbless Lema.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mpuuzi wewe mwandishi,kwani hii ni habari nzuri kiasi gani kwako mwandishi kiasi cha kuirudia mara mbilimbili?ULAANIWE,KOKO WEE!

    ReplyDelete

Top Post Ad