Chid Benz: Mpaka sasa hivi Babu Tale ameshatumia zaidi ya milioni 40 kwa ajili yangu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Moja kati ya watu anaowaheshimu rapa Chidi Benz, ni Babutale, kwasababu meneja huyo wa Diamond ametumia fedha nyingi hadi sasa kwaajili yake.

“Huwezi amini mpaka sasa hivi ninavyoestimate kwamba Tale anaweza akawa ametumia kama milioni 45, 50, 60. Sio kuwekeza, vitu ambavyo vimefanyika tayari, lakini sijasaini wala nini,” alisema Chidi kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM.

“Tale anachokifanya anaonesha kwamba ‘nia yangu mimi sio lazima tukabane kwenye suala la hela, nia yangu wewe uwe sawa, uwe okay, uwe poa.’ Kwahiyo ina maana mimi sijasaini lakini nachukulia kwamba yeye aone kusaini inawekana nikasaini ukaniletea mkataba wa miaka miwili but mimi sasa naishi na wewe kabisa,” aliongeza.

Chidi anadai kuwa anamchukulia Tale kama familia yake.

“Kwasababu hata sasa hivi nakaa kwake, bado niko kwao so yaani kwahiyo hata ukija mkataba labda aniandikie miaka 20 kwamba haina maana.”

Tale alimsaidia rapper huyo kumsaidia kuepukana na uraibu wa madawa ya kulevya ikiwa pamoja na kumpeleka rehab na baada ya kutoka kuingia studio kurekodi nyimbo mpya. Hivi karibuni aliachia wimbo wake mpya ‘Chuma’ aliomshirikisha Raymond.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad