Lema Amjibu Waziri Mwigulu. Asema Yupo Tayari Kufa Akipigania Haki Operation Ukuta

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini amemjibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kuwa Arusha tumejiandaa vyema kwa ajili ya Operesheni UKUTA, na kwamba Mwigulu siyo wa kwanza duniani kutoa lugha za vitisho duniani. Lema amesema kuwa tumejiandaa kufa ama kuuawa na Jeshi la Polisi wakipigania haki na kuikumbusha serikali kuacha kuvunja katiba ya nchi ambayo Rais na viongozi wote waliapa kuilinda.

Mh Lema ameyasema hayo kumjibu Mwigulu Nchemba aliyesema anawaonya chadema wasitingishe kiberiti, kwamba viberiti vingine vimejaa gesi.

Lema amesema kuwa kauli za hovyo zinazotolewa na serikali zinaweza kuingiza nchi kwenye machafuko. Amesema Farao Mungu alimfanya moyo wake uwe mgumu ili Apate kujitukuza mbele ya wana Israel, na kinachoonekana hivi sasa ni kwamba Mungu ameufanya moyo wa Magufuli kuwa mgumu ili Tanzania ili iweze kukombolewa.

Lema amesema kuwa hatumjaribu mtu bali wakati wa kuandamana bali tunatetea utawala wa sheria uzingatiwe, tutaandamana kutetea haki yetu ya kikatiba kufanya mikutano.

Amesema kwamba kwa sababu wamejiandaa kutupiga, nasi tumejiandaa kwa kila kitu, kwamba tunajua tarehe moja siyo siku ya harusi, kwamba tarehe moja tumejiandaa kwenda jela ama kuawa.

Tunajua tunakwenda kukumbana na polisi wakiwa na silaha na mabomu lakini tumejiandaa.

Kama Mauti imepoteza utukufu wake kwangu, hakuna statement yoyote inayoweza kurudisha Arusha kuandamana.

Amemuonya Mwigulu apime kauli zake kabla hajaitoa.

Lema amesema madai ya chadema ni madai ya msingi na endapo madai yake yatapuuzwa nchi inaweza kuingia kwenye machafuko.

Mh Lema amesema hatuandamani bei ya konyagi ipungue, bali tunaandamana utawala wa sheria katika taifa hili uzingatiwe.

Kama leo haturuhusiwi kufanya mikutano ya hadhara kwasababu rais amesema, iko siku misikitini ama makanisani itafungwa kwasababu rais amesema. Hii vita ni ya kila mtu katika taifa hili, siyo vita ya chadema

Nitakuja kumalizia baadaye kidogo nimalizie natafuta namna ya kuiweka clip hapa
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MIMI SIMO WALA SITHUBUTU.

    ReplyDelete
  2. Hamuishiwi sababu?
    Hivi kiongozi wako kuhimiza tuache siasa na tufanye kazi imekuwa nongwa,mnabadilisha maneno ili mradi tu msikike?Kweli kwamba nyie wenzetu hamuoni juhudi za rais?Kusema ukweli mimi ni mpinzani lakini siwaelewi kabisa nyie ndugu,kila kitu mnakosoa kwani kuna binadamu asiye na kasoro?SUA tupo tunawasubiri mje kama hamtakiona cha moto,na ni vizuri mkatangulia wasemaji wakuu sio kuwatanguliza walala hoi wenzetu.Mtatulazimisha mpaka tuwakosee adabu msiopenda amani wakubwa nyie.MNACHOSHA KWA KWELI AAAH!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Msenge wee
      Usiojuwa kuchamba wala kutawaza
      Wapinzani bi chachu ya maendeleo dunia nzima
      Acheni ushamba CCM
      Miaka 50 mmefanya nini Tanzania ?

      Delete
    2. Na siku mkishika dola mtatengeza dictionary
      za matusi,sasa hapo kwa nini umemtukana?kwani si
      kachangia anachokiona,au yeye sio mtanzania?
      Miaka 50 kulikuwa na mafisadi ndio walioharibu akiwemo hao mnaowakumbatia huko chadema,na sio kwamba hakuna maendeleo ila kwa kuwa wewe na kundi lako lengo
      ni kuponda kila la ccm mnajifanya hamuoni,mtakufa mmoja baada ya mmoja kwa kihoro cha kukosa madaraka.Mlaaniwe!

      Delete
  3. Huko ndio kufa kwa upinzani kwani sasa hawana hoja ila kilichobaki ni kuwahamasisha wapuuzi wenzao ati kuingia mitaani ati kupinga udikteta ambao hata wengi wa hao waandamanaji hawajui
    Hivi Dikteta huchaguliwa???
    Chadema si wajinga hivyo kwani wameona kasi ya Magufuli itauwa upinzani kabisa ndio maana wamekuja na mpango wa kuleta vurugu ili kumchafulia
    Kuwepo mpango wa kuwaelimisha watu juu ya nia ya CHADEMA

    ReplyDelete
  4. Ndugu yangu sio kulaumu Tuombe Mungu yasitokee. Tuepushe kauli yoyote ya kumuudhi mtu. Likitokea litaniumiza maana nina ndugu kila kona ya nchi hii hata wale wanaotaka kuandamana ni ndugu zangu pia wanaowaambia wasiandamane ni ndugu zangu sasa naomba kwa MUngu kisiwepo kuandamana wala kuzuia kutikisa kiberiti.

    ReplyDelete
  5. Godbless Lema wewe ni mwanaume kati ya wanaume wachache waliopo nchini,Mungu akutunze na akujalie maisha marefu na mwisho mwema

    ReplyDelete

Top Post Ad