Serikali: Mende hakubaliki kama chakula kwa jamii ya Watanzania

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baada ya utafiti wa siku chache kubaini wingi wa protini katika maziwa yanayoweza kutolewa kutoka aina mpya ya mende, Serikali imesema haina mpango wa maziwa hayo kwa sasa.

Kauli hiyo ya Serikali imekuja baada ya timu ya kimataifa ya wanasayansi kubaini chembechembe za protini ndani ya mende aina ya diploptera puntuate ambaye huzaa watoto tofauti na aina nyingine.

Mratibu wa kitaifa wa uongezaji wa virutubisho katika chakula kutoka taasisi ya chakula na lishe (TFNC), Celestine Mgoba alisema “Wala hatuna mpango wa mende kwenye matumizi ya vyakula. Ni mpaka utafiti ufanyike na Serikali itoe kibali. Inawezekana tu mtu amefanya utafiti wake, ni mpaka uthibitishwe “.

“Kitu chenyewe mende? Ukiwaambia watu kuhusu ubora wa maziwa ya mbuzi tu inakuwa shida, wengi wanataka maziwa ya ng’Ombe, ndiyo utakuja kusema mende? Halafu hao mende watatoa kiasi gani, maana yatatakiwa mengi,”alisisitiza

Mratibu wa taasisi hiyo alisema licha ya kutofahamu utafiti huo., bado mende hakubaliki kwa jamii ya Watanzania kama chakula.

BY: EMMY MWAIPOPO
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Acheni uzushi mmekazania mende mende hata huku nje hawazungumzia kuhusu maziwa ya mende.Wakianza kunywa nchi za magharibi ndio mtaanza kuzungumzia.

    ReplyDelete

Top Post Ad