Wanaowabeza Polisi Mitandaoni ‘Kushughulikiwa’

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

JESHI la Polisi limefura. Ni kufuatia watu mbalimbali kulibeza mitandaoni kwa madai kuwa, limejikita katika matamko na mazoezi ya kukabili maandamano ya vyama vya siasa vya upinzani, kuliko kujipanga kukabiliana na uhalifu mkubwa ukiwemo ujambazi, anaandika Pendo Omary.

Askari wanne waliuawa katika tukio la ujambazi lililotokea usiku wa jana, eneo la Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam na kuibua maoni tofauti ya wananchi katika kipindi hiki ambacho polisi wamekuwa wakijitokeza mitaani na kufanya maonyesho kwa madai ya kujiweka tayari kuwakabili wahalifu.

Nsato Marijani, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi hapa nchini amewambia wanahabari hii leo kuwa, jeshi hilo halitavumilia ‘ushabikiaji’ wahalifu unaofanywa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii huku wakilibeza jeshi la polisi.

CP Marijani aliwaita wanahabari ili kuzungumzia mazingira ya tukio la kutokea kwa mauaji ya askari wa jeshi hilo siku ya jana, ambapo amesema, kitendo kilichotokea jana sit u ni uhalifu bali ni “tangazo la vita dhidi ya Polisi”.

“Wahalifu walifanikiwa kupora bunduki zetu mbili aina ya SMG na risasi 60 na hawakuchukua pesa wala kuharibu mali yoyote ya benki hiyo. Maana yake wahalifu hao walilenga kuwashambulia askari polisi wetu,” amesema na kusisitiza;

“Inashangaza kuona baadhi ya watu wanashabikia uhalifu kutokea kupitia mitandao ya kijamii na natoa onyo kali kwao, waache kuhamasisha uhalifu maana tunawasaka, tutawakamata na kuwahoji ili sheria ichukue mkondo wake.”

Jeshi hilo limesema, tayari limewakamata baadhi ya watu wakihusishwa na mauaji hayo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni kukosa utu na hofu ya Mungu.Mimi ni mpinzani lakini kamwe siwezi kufurahia mauaji ya askari wetu.Hata wanyama wanaofanana wakiona mwenzao mmoja kafa husononeka sembuse sisi binadamu wenye utu.R.I.P makamanda wetu.

    ReplyDelete
  2. Msitishe watu hapa
    Anasemwa papa ,
    Obama ,
    Malikia
    Hakuna anayeshabikia mtu kufa
    Ila watu wana wambia ukweli polisi mmekuwa wanasiasa
    Inashangaza kila kukicha mpo kwenye media kana kwamba ni waandishi wa habari
    Kila kukicha
    Uchochezi
    Uvunjifu wa Amani
    Interijensia
    Hamjawa wabunifu hata siku moja jinsi ya kukabiliana na ujambazi
    Wamekuwa wakiumia ni polisi wa ngazi chini nyinyi wakubwa kazi kutuoa amri
    Kumbukeni Tanzania si ya CCM pekee
    Na polisi kuna wana ukawa
    Siasa waachieni wanasiasa

    ReplyDelete
  3. Hahahahahhahaha....au na kucheka pia haturuhusiwi...maaana daaah..

    ReplyDelete
  4. Haya! Mie napita2

    ReplyDelete
  5. Kwa hiyo mitaandao ni ya polisi pekee kuonyesha vifaa vyao vyakupbana na wahalifu?
    Hivi kuandamana ni uhalifu
    Kazi yenu ni kulinda maandamano na siyo kuamua nani aandamame
    Mmetutoka watanzania
    Hatuna Imani nanyi kwa ajili ya watu wachache badilikeni
    Najuwa tupo tuandikao ukweli halisi
    Msiwe wanasiasa
    Nchi nyinyi zimeingia kwenye machafuko baada ya polisi kugeuka kuwa wanasiasa

    ReplyDelete

Top Post Ad