Picha: Mkubwa Fella aonyesha nyumba 4 za wasanii wa Yamoto Band ‘watu wanaongea sana’

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkurugenzi wa Yamoto Band, Mkubwa Fella ameonyesha nyumba nne za wasanii wake wa Yamoto Band baada ya baadhi ya watu kuhoji kuhusu mafanikio ya wasanii hao.
Nyumba nne za wasanii wa Yamoto Band
Nyumba nne za wasanii hao

Akiongea na Bongo5 Ijumaa hii akiwa Mbande Kisewe, Chamazi jijini Dar es salaam, Fella amesema ameamua kuonyesha nyumba hizo baada ya kuchoka maswali ya watu kuhusu mafanikio ya wasanii hao.


“Leo nimewaita hapa Mbande Kisewe siyo kuzindua ila kuwaonyesha kwa sababu kuna meseji nyingi nazipata, Mkubwa vipi mbona watoto wananenepa wanavaa vizuri, maendeleo vipi, mbona kuna wasanii wamekuja juzi tu, tunawaona wanafanya vitu vikubwa. Kwa hiyo nimewajengea hizi nyumba lakini bado hazijazinduliwa, nataka uzinduzi wake Mh rais mtaafu Kikwete aje azindue na kuwakabidhi hawa vijana nyumba zao,” alisema Fella.

Aliongeza, “Kwa hiyo nataka wale wanaosema Yamoto wananini waone nini kimefanyika, kwa sababu nilikuwa natengeneza kitu kikubwa, siyo vibanda majumba na mlivyoyaona. Kwa hiyo 80% nyumba zimekamika, kuna vitu ambavyo sijamalizia kwa sababu kila mtu najua atataka kuweka manjonjo yake kwenye nyumba yake, kwa hiyo ndani ya miaka mitatu tulichovuna tumekiwekeza kwenye hizi nyumba, ni kubwa naza kisasa kabisa,”

Meneja huyo siyo mara yake ya kwanza kuwajengea wasanii wake nyumba, alishafanya hivyo kwa Temba na Chege pamoja Juma Nature. Angalia picha.

Source:Bongo5
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Weka wazo kipato na jinsi pesa zilivyopatikana ndicho watu wanachotaka kujua. Show your income. Je kinaendana na pia malipo ya kodi. Au ni madili ya awamu ya nne anayoongelea Magufuli. Na kwa nini Kikwete ahusishwe na uzinduaji huu. Kuna uhusiano gani kati ya Kiwete na maswali unaypulizwa. Au kuficha ukweli wa mambo.

    ReplyDelete
  2. Kazi nzuri sana tena naomba jibu mimi ni muangaikaji hizo nyumba tatu garama yake ni shilingi ngapi?? Naomba jibu tafadhali.

    ReplyDelete
  3. kazi wanazozifanya je zinalingana na Gharama (thamani)ya hizo nyumba au una walalia na wewe unachukua kikubwa zaidi!!?

    ReplyDelete

Top Post Ad