Waziri Mkuu Majaliwa Akwama Kuhamia Dodoma

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

SERIKALI Mkoa wa Dodoma imesema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atahamia rasmi mkoani humo mara baada ya kumalizika kwa vikao vya Bunge vinavyoanza wiki ijayo, Septemba 6.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema baada ya kufika Dodoma, ataanza kuratibu utaratibu wa wizara mbalimbali kuhamia katika Makao Makuu hayo ya nchi.

Pamoja na hayo Jeshi la Polisi limejipanga kuongeza vituo vya Polisi ili kuimarisha ulinzi wakati serikali itakapohamia na hakuna mwananchi atakayenyang’anywa ardhi yake kwa sababu yoyote ile.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, Rugimbana alisema kama mkoa walishauri ujio huo ufanyike mara baada ya kikao cha Bunge na Waziri Mkuu ameridhia suala hilo.

Alisema Waziri Mkuu atakuwa Mratibu wa wizara zote kuhamia Dodoma na kazi hiyo ataianza rasmi mara baada ya kuwasili mkoani humo.

Alisema maandalizi yanaendelea vizuri na ukarabati wa nyumba ya Waziri Mkuu umefikia asilimia 90.

Alisema Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christine Mndeme aliyekutana na makundi mbalimbali kwa ajili ya mapokezi ya Waziri Mkuu.

“Awali tulisema atakuja Septemba Mosi lakini baada ya kushauriana tumeona aje mara baada ya vikao vya Bunge kwani pilikapilika nyingi zitakuwa zimepungua, kama serikali ikiamua kuja leo tutaipokea kwani maandalizi ya serikali kuja Dodoma yamekamilika kwa asilimia 70,” alisema.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwanini wasishauriane kabla ya matamko yao kuwa atahamia sep 1?

    ReplyDelete
  2. Karibu sana Mh Majaliwa. Dodoma mnakarishwa waheshimiwa kwa nyoyo zetu kunjufu na tuaahidi kushirikiana nanyi kwa hali na Mali.. Milango yetu iko wazi na familia zetu zinafuraha kuona ndugu zetu. mnakuja kuungana nasi katika ushirikiano wa maisha hapa kwetu na ni kwenu karibuni sana na wakati wowwote saa yoyote.Jihisini mko nyumbani.. Karibuni Sana.

    ReplyDelete
  3. Kama kaiwaida ya awamu ya tano kukurupuka na kuropoka kabla ya kufikiri
    Fyuuuuuuu
    mtaumbuka fikirieni kwanza kabla ya kusema
    wajinga na wapumbavu uta wajuwa tuuuu
    vishindo vyote pesa ya huhamia hamna
    Hata ROM haikujengwa kwa mwaka
    Mfupa aliushindwa fisi mbwa atauweza ????
    Kuhamisha makao makuu yanataka pesa na plan
    mmetubia pesa zetu miaka yote
    watu wanna nyumba dar na Dodoma
    fyuuuuuuu
    Tanzania ni nchi pekee duniani yenye makao makuu mawili
    Pamoja na kuwa nchi maskini duniani

    ReplyDelete

Top Post Ad