UVCCM Waichokonoa Chadema, Wadai Wana Siasa za Maigizo Baada ya Kushindwa Kufanya Operesheni UKUTA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umewavaa viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kile walichodai kuendesha siasa za maigizo baada ya kushindwa kuzindua Operesheni UKUTA, Septemba 1.

Kupitia taaria yake kwa vyombo vya habari, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, amesema kuwa Chadema walijua kuwa hawana ubavu wa kufanya maandamano na mikutano nchi nzima Septemba 1 na kwamba walichofanya ni kuwatia hofu wananchi.

“UVCCM tulijua, tulielewa na kutambua bayana kwamba Chadema walikuwa wanafanya maigizo katika siasa, hawana ubavu wala jeuri ya kuandamana kwa madai ya kipuuzi na ambayo sio ya msingi kwa mustakabali wa nchi yetu,” alisema Shaka.

Aidha, Shaka alikanusha sababu zilizotolewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuahirisha maandamano hayo kuwa wameombwa na viongozi wa dini ili waweze kukaa na pande zote kujaribu kutafuta suluhu kwa amani.

“UVCCM inatamka bayana kuwa hakuna majadiliano, mazungumzo wala mijadala itakayojadiliwa kati ya Serikali ya CCM na Chadema. Tunaomba Serikali ya Rais John Magufuli iendelee na mikakati yake ya kisera,” Shaka ameongeza.

Kaimu Katibu Mkuu huyo wa UVCCM alisisitiza kuwa Chadema hawana ubavu wa kufanya maandamano na mikuano nchi nzima Oktoba 1 kama walivyosema, baada ya kushindwa kufanya hivyo Septemba 1.

Shaka amesema wanachokifanya hivi sasa Chadema kinatokana na kushindwa kubuni mikakati ya kufanya siasa ili chama chao kiimarike na kukubarika.

Juzi, Chadema walitangaza kuahirisha uzinduzi wa oparesheni UKUTA nchi nzima, iliyokuwa imepangwa kufanyika jana (Septemba 1) kwa maandamano na mikutano nchi nzima.

UVCCM pia walitangaza kuahirisha maandamano yao ya nchi nzima waliyokuwa wamepanga kuyafanya Agosti 31 kwa lengo la kumpongeza Rais Magufuli kwa kazi aliyoifanya ndani ya kipindi kifupi.

Maandamano ya pande zote mbili yalipigwa marufuku na Jeshi la Polisi nchini.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivi Ccm mna nini?mbona mnakuwa wachokonozi na kama wtoto wadogo .lakini hamshikwi na polisi na raisi yuko kimya. Mtutumika kuleta vurugu na mmkikingiwa kifua na chama na raisi na kutumia polisi.maneno yenu ya dharau, chuki, uchochezi hayana mwanzo wala mwicho. Kwa nini mnaruhusiwa kuchochea mambo?

    ReplyDelete
    Replies
    1. UCHOCHEZI AU VURUGU GANI?KWANI UVCCM NDIO WALIOWAAGIZA MJENGE UKUTA?NI CCM TU NDIO WAMEPINGA UKUTA?MBONA VIKO VYAMA VINGINE VYA SIASA VIMEPINGA UKUTA.SWALI KWA NINI CHADEMA MNAPENDA KUPINGA KILA KITU?KUHAMIA DODOMA WAMEKURUPUKA,UNUNUZI WA NDEGE WAMEKURUPUKA,ELIMU BURE WAMEKURUPUKA,KILA KITU KINACHOFANYWA NA SERIKALI KIBAYA,NYIE NI WAPINZANI GANI,NA KWA NINI NYIE TU?
      SHIME TUFANYE KAZI,TANZANIA KWANZA!

      Delete
    2. Wanafiri wtz hatuna akiri!!! wajifunze kutoka Gabon nini kinaendelea sasa hivi!!!

      Delete
  2. HAYO MANENO YA SHAKA WA UVCCM ...NI UCHOCHEZI MTUPU . KWA NINI HAMTULII

    ReplyDelete
  3. Huyu Mzanzibari mbovu Shaka anapenda kujitia kimbelembele kama mgongo wa pua! anafikiri atawaonea waTanznaia kwa kejeli zake kama anavyofanya kule Pemba.

    ReplyDelete
  4. Wape wape vidonge vyao hao, wakitema, wakimeza WATAJIJU........HAPA KAZI TU! Hebu wajaribu kuandamana wakione kilichomnyoa kanga manyoya ya shingoni

    ReplyDelete
  5. Hivi siasa kumbe ni taarabu

    ReplyDelete
  6. Ashikiwae apiga , sima shujaa Wa kondo.....waswahili walisema uvccm ....!!!

    ReplyDelete
  7. Wasenge wote hao wanatoa migongo kwa vigogo wa CCM

    ReplyDelete

Top Post Ad