CUF Tanga Wamgomea Profesa Lipumba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

CHAMA cha Wananchi (CUF) wilayani hapa kimetoa tamko la kutomtambua Mwenyekiti wa Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, na kwamba hakitampokea katika ziara yake.

Lipumba anatarajia kuanza ziara mkoani Tanga kesho  huku uongozi wa chama hicho ukisisitiza kutambua uamuzi wa  Mkutano Mkuu uliomwondoa madarakani na wa Baraza Kuu kumvua uanachama.

Mwenyekiti wa CUF wa Wilaya ya Tanga, Rashid Jumbe alitoa tamko hilo jana akieleza kuwa hawatakuwa tayari kukaidi Katiba ya Chama chao na kwamba hawatampokea na hakuna maandalizi yatakayofanyika kumpokea.

"Tumeambiwa Lipumba ana dhamira ya kufanya ziara mkoani hapa. Sisi kwa uamuzi wa Baraza hatumtambui, wala hatujaandaa maandalizi ya kumpokea.

“Wilaya za Korogwe na Muheza ndizo zimesema atazitembelea, lakini sisi hatuko pamoja nao na watakaompokea wataingia kwenye mgogoro mwingine kwa sababu hatambuliki," alisema Jumbe.

Mwenyekiti huyo pia alizungumzia mgogoro baina yao na CCM kutokana na sakata la umeya ambapo alisema  hatima ya mgogoro huo itajulikana baada ya mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29.

Alisema kutokana na sakata hilo walitoa malalamiko kwa viongozi mbalimbali lakini hakuna hatua zozote zinazoendelea, hivyo Kamati ya Utendaji iliwataka madiwani wa chama hicho kutohudhuria kikao chochote cha Halmashauri hadi itakapotoa uamuzi.

"Tumetoa malalamiko yetu kwa viongozi wa CCMna lengo letu ilikuwa tuonane na  Rais lakini tulimpata Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa aliyetwambia kuwa atalifanyia kazi, lakini sasa tumeamua kupeleka malalamiko yetu kwa wenye chama na wao ndio watakaotoa uamuzi juu ya mgogoro huo.

“Hivyo tumeitisha mkutano ambao utakuwa na wajumbe 440 ambapo tuna imani kuwa tatizo letu litakwisha Oktoba 29,” alisema Jumbe.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lipumba ni mwenyekiti halali na ana uwezo wa kupangua uongozi wa mkoa na kutoa majukumu kwa atakao wachagua hapo mkoani...Mpeni ushirikiano anao stahiki kama kiongozi mkuu wa Cuf -Bara

    ReplyDelete
  2. Enter your comment...hawezi kuwa mwenyekiti alisha kimbia kwanza mwenyekiti anatakiwa awe na akili timamu awejasiri na ajiamini sasa huyo sizani kama anauwezo wowote

    ReplyDelete
  3. Bwana Yule hajielewi, kwann anageukageuka kama kinyonga?
    Inamaana alikua anakusudia nn alipo jiuzulu?
    Anatakakuwafanya watu mazezeta?

    ReplyDelete

Top Post Ad