MAMA Profesa Tibaijuka Apewa Tuzo Nyingine ya Kimataifa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Profesa Anna Tibaijuka
ALIYEWAHI kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ametunukiwa tuzo baada ya kutangazwa mshindi wa mwaka 2016 wa Taasisi ya Mafanikio ya Govan Mbeki (Govan Mbeki Lifetime Achievement Award), katika sherehe iliyofanyika usiku wa kuakia jana, kwenye Ukumbi wa International Convention Center (ICC) mjini Durban, nchini Afrika Kusini.

Profesa Tibaijuka, ambaye pia alipata kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN- Habitat), ametunukiwa tuzo hiyo kutokana na ufanisi aliouonyesha, ikiwa ni  pamoja na kuendesha mikakati na kampeni kubwa bila kuchoka ya kupambana na makazi duni na mazingira barani Afrika na duniani,  wakati akiliongoza shirika hilo.

Waziri wa Maendeleo ya Makazi wa Afrika Kusini, Lindiwe Sisulu, ndiye aliyemkabidhi tuzo hiyo na cheti Profesa Tibaijuka, baada ya kutangazwa mshindi.

Profesa Tibaijuka, ambaye ni Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), ametunukiwa tuzo hiyo baada ya kuonyesha kuthamini mchango wake wakati akiwa UN Habitat, kati ya mwaka  2000-2010.

Kiongozi huyo, licha ya kujipatia sifa lukuki wakati akiliongoza shirika hilo la Umoja wa Mataifa na hivyo kumuandalia njia nyepesi ya kushinda ubunge Jimbo la Muleba mwaka 2010 na hata kuteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, hata hivyo, sifa hizo zilitiwa doa baada ya kuhusishwa kwenye mgawo wa fedha tata zilizochotwa kutoka katika akaunti ya Escrow.

Profesa Tibaijuka, licha ya mara kadhaa kujitetea kwamba fedha hizo alipewa kwa ajili ya shule yake, baadhi wamekuwa wakidai kuwa kitendo hicho kimemuonyesha kuwa si mtu safi na anayestahili kuaminiwa.

Kwa maneno yake mwenyewe, Profesa Tibaijuka amekuwa akidai kuwa hayo anaonewa na kwamba hata kupokea kwake fedha hizo kumegeuzwa kuwa ni dhambi na wapinzani wake wa kisiasa.

Kutokana na hayo, wakati fulani alisikika akiunga mkono mpango wa Rais John Magufuli kuanzisha mahakama ya mafisadi.

Profesa Tibaijuka alisema chombo hicho kitachangia kutoa haki na kuweka ukweli bayana, kwakuwa watuhumiwa wengi wa ufisadi wanatolewa kafara.

Alisema  akiwa kama mmoja wa wahanga wa tuhuma za ufisadi,  kuanzishwa kwa mahakama hiyo kutasaidia, kwakuwa kuna kundi la watu ambalo linatolewa kafara na mafisadi ili kuficha madhambi yao.

“Ukishaanzisha mahakama ya mafisadi unatafuta haki na ukweli, Watanzania ni wepesi wepesi wa kuamini, Watanzania tuhuma tu wanaona tayari umeshakuwa convict (hatiani), mimi ni mmoja wa wahanga wa tuhuma za ufisadi na nilituhumiwa bila kuwa na uhakika, kuna mitandao ya mafisadi wenyewe wanahakikisha hawakamatwi na badala yake wanawapeleka wengine mbele ili wawatoe kafara,” alikaririwa Profesa Tibaijuka.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa nini nchi za Ulaya zinawatunukia vyeo waafrica wanaoshirikiana nao.
    Wanafaidika. Miaka kumi Tanzani ifisadi, ESCROW, utoaji ardhi mwa wageni , kunyang"anywa wsmassai ardhi wao wanaona ni maendeleo. Comflict of interests. Africa itachukua muda viongozi wetu bila kutumika na vibarska ingawa tumaelmu za juu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanawapenda viongozi corrupt ili, nchi za Africa ziendelee kidhalaulika pamoja na watu wake, wadhalaulike popote pale duniani, ndio maana watafanya Kila mikakati, kuwapongeza, viongozi wanaolingusha bara la Africa, lisisonge mbele, waendelee kulita bara na nchi za dunia ya tatu, bara masikini, na linalongoza kwa magonjwa, lisilokuwa , na maendeleo na viongozi, wabovu, wanaowaibia wananchi wao, wachoyo, wenyeIQ ndogo, yaani uwezo wao wa kiakili ni mdogo, haliwezi kuendelea

      Delete

Top Post Ad