Nilifanya Collabo na AliKiba Nipate Ugali-Ommy Dimpoz Afunguka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa amerudi kwenye game na kolabo ya wimbo wa 'Kajiandae' aliyofanya na Alikiba tena, ametoa sababu ya kuamua kufanya tena kollabo na msanii huyo.

Akizungumza kwenye FNL ya East Africa Television na East Africa Radio, Ommy Dimpoz amesema mara ya kwanza alivyofanya kollabo ya Nai Nai na Alikiba ilikuwa ili atoke kimuziki, lakini kollabo ya sasa ni kama tu collabo zingine, na sio kumtumia kurudi kwenye game.

"Nai nai ilikuwa mimi nimemshirikisha Ali nilikuwa natafuta njia ya kuuona ugali, lakini sasa hivi tumekuja kama Ali na Ommy kazi ya pamoja, mimi nilikuwa zangu break, nimerudi kwa hiyo haijalishi nimeimba na nani", alisema Ommy Dimpoz.

Ommy Dimpoz alishawahi kumshirikisha Alikiba kwenye wimbo wa 'Nai nai' ambao ndio ulimtambulisha kwenye ulimwengu wa bongo fleva, na sasa kaamua kurudi na kazi nyingine akiwa na alikiba pia, inayoitwa 'Kajiandae'.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad