RUGE "Tulisha Maliza Bifu na Lady Jay Dee, Tunasubiri Ruksa ya Kucheza Nyimbo Zake tu....

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ruge Mutahaba amesema siku Lady Jaydee akiwaambia waanze kucheza nyimbo zake watafanya hivyo.

Bosi huyo wa Clouds Media Group, ametoa kauli hiyo Ijumaa hii kwenye mahojiano na kipindi cha XXL cha kituo hicho. “Tatizo ni kwamba hakuna ambacho hatujamaliza, tulimaliza, tunasubiri order. Unajua kimsingi ulipopewa order ya kwamba ‘nyimbo zangu usipige, jina langu usiseme kwenye chombo chako, vyovyote itakavyokuwa mimi sitaki kusikia hiyo kitu’ hiyo ndio order. Kwahiyo labda tukikutana, nimuombe tena @jidejaydee kama tutaruhusiwa kufanya hiyo kitu,” alisema.
Ruge amesema ana muda mrefu hajawahi kukutana na Lady Jaydee, japo amedai ‘hata leo nikipata nafasi ya kahawa nitashukuru sana kwa huo mwaliko.’
.
Wiki kadhaa zilizopita Ruge na Joseph Kusaga walishinda kesi ya kuchafuliwa (defamation) iliyokuwa imefunguliwa dhidi ya #LadyJaydee na muimbaji huyo kuamriwa kuwaomba radhi.
.
“Tunashukuru walau tulishinda ile kesi lakini at least ilitengeneza mfano wa watu kuelewa kwamba tusipende kutuhumu vitu kama watu huna uhakika. Bahati nzuri pia hata katika hiyo kesi alisema mwenyewe hajawahi kusikia tunasema, aliambiwa na watu. Lakini ni mambo yashapita hayo.”

Sikiliza Hapa:

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad