FUNDI Pancha Atupwa Jela Miaka 30 Kwa Kukutwa na Misokoto 601 ya Bangi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Fundi wa kuziba pancha, Harson Solomon (38), mkazi wa wilayani hapa amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kupatikana na misokoto 601 ya bangi.

Kifungo hicho kimeangukia sheria mpya ya udhibiti wa dawa za kulevya iliyosainiwa Mei 11, 2015 na aliyekuwa Rais wakati huo, Jakaya Kikwete. Imeelezwa Solomon ni miongoni mwa washtakiwa wa mwanzo kufungwa kwa sheria hiyo.

Awali, sheria ilikuwa inatoa mwanya wa faini na mtu anaposhindwa kulipa ndipo hutumikia kifungo jela lakini hivi sasa anayepatikana na hatia ya kukutwa na kiwango kikubwa hutupwa jela.

Kifungu cha 11(1) D cha sheria hiyo mpya, kinaeleza wazi mtu anayezalisha, kumiliki, kuuza, kununua au kusafirisha dawa za kulevya ikiwamo bangi, adhabu ya chini ni kifungo cha miaka 30 jela.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Joachim Tiganga baada ya kuridhishwa bila kuacha shaka na ushahidi wa upande wa mashtaka.

Wakili wa Serikali, Ignas Mwinuka alidai kortini kuwa Desemba 1, 2015 katika maeneo ya Mwika Kimangara, Moshi Vijijini mshitakiwa alipatikana na kiasi hicho cha bangi.

 Pia, anadaiwa kuruhusu eneo lake kutumika kuuza bangi na gongo.

Akisoma hukumu, Hakimu Tiganga alisema matumizi ya dawa za kulevya yanazidi kuongezeka nchini na kuathiri jamii, hivyo Mahakama inatoa adhabu hiyo iwe fundisho kwa wengine.

Katika kipindi chote tangu afikishwe kortini kwa mara ya kwanza Desemba 11 mwaka jana, mshtakiwa alikana mashtaka hadi alipotiwa hatiani na kuhukumiwa jana.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nasikia kutapika kwa kifungo mijizi iliyoiba mabliioins inatesa mittani
    Nafikiri huyu Hakimu atumbuliwe huenda aliomba rushwa akakosa
    Bangi Leo hii dunia nzima inaanza kurusu bangi na maduka rasmi yapo
    Bangi inasemekana inatumika kutibu maradhi mbali mbali

    ReplyDelete
  2. mdau hapo juu umenena, mijizi ambayo imeuwa watu na kuiba mamilioni ya hela haikamatwi lakini jamaa kakamatwa na bangi ambayo kwenye nchi za wenzetu zinauzwa kwenye migahawa na kule marekani watu wanaandikiwa na daktari kama dawa ya kutibu magonjwa au kutuliza makali ya magonjwa halafu bongo mtu kakamatwa nayo anapelekwa jela kusota miaka 30 huo ni uonevu wa hali ya juu kwanza bangi haijawahi kuua mtu

    ReplyDelete
  3. na hao wanaokamatwa na unga kesi zao huwa zinaishia wapi mbona hatujawahi kusikia wale waliokamatwa na unga kuwa wamehukumiwa ni kwanini? sababu wanahela wametoa rushwa na wameachiwa mnawaonea kuwafunga wa bangi tu sababu hawana hela ya kutoa rushwa

    ReplyDelete

Top Post Ad