AFA Baada ya Kufakamia Pombe ya Kienyeji

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Bahati Mbula (43) mkazi wa Kanindo Kata ya Kishiri amefariki dunia kwenye mkesha wa mwaka mpya baada ya kudaiwa kunywa pombe za kienyeji kupita kiasi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema hilo ni tukio pekee lililotokea katika mkesha wa mwaka mpya mkoani Mwanza.

“Nimepata taarifa moja tu ya mtu mmoja kufariki huko Kanindo, marehemu huyo anadaiwa kunywa kwa kuchanganya pombe za aina nyingi za kienyeji.

“Nimeambiwa marehemu huyo alitoka eneo la Sawa Kata ya Lwahnima na kwenda kunywa huko Kanindo, sasa usiku huo wenzake walidhani ameondoka kurudi kwao kumbe alikuwa ameanguka  njiani karibu na pale alipokuwa akinywa pombe hiyo,” alisema Kamanda Msangi.

Alisema Jeshi la Polisi linafuatilia kwa uchunguzi zaidi kama alikuwa anaumwa au kuna kitu kingine.

“Tuliwaambia wananchi washerekee  mwaka mpya bila kuleta madhara yoyote ikiwamo kuchoma moto matairi, kuendesha magari ovyo,  kurusha mawe nadhani watu walizingatia ndiyo maana hata matukio ya uhalifu hayakuwapo,” alisema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. inafahamika kuwa wasukuma ni walevi kupita kiasi kila mara tukio la pombe likitokea ni Mwanza, juzi juzi kondakta wa basi alifukuzwa kazi sababu ya kulewa na kuzimika wakati wa kazi huko Mwanza, pia wasukuma wanaoishi huku majuu ni walevi sana wanakunywa pombe mpaka makazini

    ReplyDelete

Top Post Ad