Dokii Afunguka Kumpenda Mwanamuziki Darasa...Adai Yupo Tayari Kuolewa Naye

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii wa filamu, Dokii ameamua kufuata nyayo za Stereo kwa kuamua kumchana rapper Darassa kuwa anampenda.


Muigizaji amedai kwa sasa anamkubali sana Darassa kupitia kazi yake ya muziki, lakini yuko tayari kuolewa naye endapo Darassa mwenyewe atahitaji hilo.

“Nampenda sana Darassa, i love him, nampenda kwa sababu ya kazi yake, lakini sijawahi kumwambia, he is handsome….Darassa mi nampenda kazi yake but is very handsome, so what do you expect?… Mie sina mtu kwa sasa, so kama Darassa akitaka kunioa, niko tayari, am ready coz he is handsome” Dokii alikiambia kipindi cha FNL cha EATV.

Dokii alisema hayo ili kufafanua kuhusu picha ambayo ameonekana akiwa amepiga na Darassa, picha iliyozua mjadala kutokana na kuwa katika pozi lenye utata.

Pia alifafanua kuhusu mahusiano yake na msanii Rich Mavoko, ambapo alisema Rich ni ndugu yake hivyo hawawezi kuwa wapenzi.

Wiki chache zilizopita, rapper Stereo alimchana rapper Chemical kuwa anampenda na yupo tayari kwa lolote.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Duh! Shida, Dokii ujana wako uliumaliza wapi na uzee unataka kumkomaza mtoto wa watu. Mbona hujasema kitambo kama unamzimia? Ndio kwanza ujue kuwa handsome?

    ReplyDelete

Top Post Ad