Lowassa Akerwa na Gazeti Lililoandika Uongo Dhidi Yake, Adai ni Mbinu Chafu Zinazofanywa na CCM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri  Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, amesema kasi ya kuimarika kwa umoja na mshikamano miongoni mwa vyama vya upinzani nchini, kunaitia kiwewe CCM kiasi cha kuanzisha mbinu chafu za kisiasa.


Kauli hiyo aliitoa jana mjini Kahama katika Hoteli ya Gaprina ambapo alifikia kabla ya kuanza safari ya kuelekea mkoani Kagera katika ziara ya kuimarisha chama chake.


Alisema kuimarika kwa mshikamano huo chini ya mwavuli wa Vyama Vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi  (Ukawa) ni hatua kubwa katika kuelekea kuing’oa CCM.


“Wameanza mbinu zao za kutaka kutuondoa katika umoja wetu, wameanza kuwalisha viongozi wetu maneno, mfano  gazeti (nalitaja jina) la leo (jana) wamenilisha maneno ya kwamba eti nimeitabiria CCM ushindi katika uchaguzi mdogo wa udiwani kule Arumeru.


“… mambo ya ajabu kabisa hili  gazeti linaishi kwa kodi zetu sisi wananchi leo linaamua kutumika kuvunja demokrasia inasikitisha sana.


“Wanaandika uongo mchana kweupe kuwa nilikuwa katika kampeni kwenye kitongoji Ematasia..mimi sikwenda huko..lakini mbinu zao hizi wananchi wameshazijua na hawako tayari kuona hamu yao ya kupata mabadiliko inapotea,” alisisitiza.


Wakati huo huo mamia ya wakaazi wa mji wa Kahama waliizingira Hoteli ya Gaprina alikofikia Lowassa, wakiwa na nia ya kutaka kumwona.


Akiwa njiani kuelekea Bukoba, Lowassa na msafara wake alipata nafasi ya kusalimiana na wananchi katika mnada wa Lusaunga wilayani Biharamlo, ambako wananchi hao walimwambia kuwa hali yao ya maisha ni ngumu pamoja na hali mbaya ya ukame inayowakabili.


Hata hivyo Lowassa hakutoa kauli yoyote kwao zaidi ya kusema kwa sasa mikutano ya hadhara imepigwa marufuku na asingependa kuvuja sheria kwa kile alichodai amri kandamizi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. SAAAAFI SANA ILA SAFARI HII USIGOMBEE URAIS.
    CHAGUENI MTU MWINGINE WEE PIGA DEBE TU KWAKE ATAKAESIMAMA.

    ReplyDelete
  2. Hoja ya Lowassa ni hafifu sana. Anatoa hoja hiyo huku akijua (au pengine hujui) kwamba watanzania wengi wazalendo wanamwogopa kama ukoma kwa uchu wake wa kukimbilia Ikulu bila sifa stahiki.
    Kwanza anachokifanya hapa ni propaganda za kisiasa kujitafutia tu umaarufu lakini azingatie kwamba wanaCCM na watanzania wengi ni waelewa wanahitaji viongozi walioshiba kimaadili na wengi wao tena wote wako CCM.
    Chama Cha Mapinduzi hakiwezi kuweweseka kwa kitu cha umoja wa upinzani ambacho hakipo.
    Kitu cha umoja kwa mwenye akili anajua kwamba hata wahuni wanao umoja wao. Makundi ya namna hiyo ya kihuni kama ni ya kisiasa basi huwa ni hatari sana kwa mustakabali mwema wa taifa kama yatapewa nafasi katika mifumo muhimu ya nchi.
    Watanzania wote tujifunze kuwatambua chui waliovaa ngozi za kondoo.
    Tumetoka mbali hatutaki magugu mabaya.
    #usirudiekosa2020kupigiakuraupinzaniovyo.
    #CCMdaima.

    ReplyDelete

Top Post Ad