Oh Nooh!! Mamilioni ya Mtoto wa Pili wa Diamond Yatoweka Kimiujiza,Mwenyewe Asema Hilo Halimsumbui..!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Matarajio ya mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ya kumtumia mwanaye Nillan kupata mamilioni ya pesa kutoka kwa wadhamini yanadaiwa kubuma kufuatia maelezo kuwa, baadhi ya makampuni yaliyokuwa yamezungumza naye yameamua kujiweka pembeni kutokana na ukata wa pesa.


Awali, akizungumza  hivi karibuni, Diamond aliweka wazi kuwa, kabla hata mtoto hajazaliwa kuna benki mbili ambazo zilimwaga dau la mamilioni ya pesa kwa ajili ya kutumia picha ya mtoto huyo kwenye huduma zao lakini yeye alikuwa hajaweka wazi ipi aingie nayo mkataba na kwa mkwanja upi.

Diamondakiwa amembeba mwanaye mchanga, Nillan.
Hata hivyo wakati mtoto huyo akikaribia kufikisha mwezi mmoja, taarifa zilizotufikia zinadai kwamba baadhi ya makampuni yaliyojitutumua kutaka kutoa mamilioni kwa ajili ya sura ya mtoto huyo yameingia mitini.

Chanzo makini kilicho karibu na msanii huyo kilidai kuwa, awali Diamond alikuwa amefanya mazungumzo na makampuni na mabenki tofauti lakini kutokana na hali ngumu, baadhi wamekaa kimya mpaka sasa.

“Kimsingi yale mamilioni ambayo Diamond na Zari walitarajia kuyapata kutoka kwa makampuni na benki kama ilivyokuwa kwa Tiffah, yamebuma. Mambo yamekuwa siyo.

“Inavyoonekana huku kubana pesa za dili kwa Rais John Magufuli kumewafanya hata wale waliokuwa wakitaka kutoa pesa ili wanunue sura ya Nillan wafanye uamuzi wa kupotezea.”
zari-na-mond-kidZari (aliyelala) ikiwa ni saa chache baadea ya kujifungua

Umaarufu wa Nillan umechangia?

Aidha, wachambuzi wa mambo wameeleza kuwa, kubuma kwa mapesa hayo kunaweza kuwa kumetokana na mtoto huyo kutovuma kama ilivyokuwa Tiffah hivyo kuna ambao wameona kutoa pesa kwa ajili ya sura yake ni sawa na kuzitupa.

“Kipindi cha Tiffah ilikuwa rahisi sana benki na makampuni mbalimbali kutoa pesa ili kununua sura yake kwa kuwa alikuwa ‘hot’ na pia fedha ilikuwa inapatikana kirahisi lakini ikimbukwe huu ni utawala na Magu, pesa haitoki kirahisi.

“Pia Nillan mpaka sasa hawezi kuishawishi benki yoyote itoe mamilioni kununua sura yake kwa kuwa hana kiki kivile. Kwa mfano Tiffah alipozaliwa na kufunguliwa ukurasa wake wa Insta, ndani ya siku mbili tu alikuwa na followers (wafuasi) 200,000 lakini kwa Nillan akiwa anakaribia kufikisha mwezi mmoja ana followers 69,000, hiyo inaonesha watu hawamshobokei na hata kibiashara sura yake haiwezi kuwa kivile,” alisema Rashid Maguli wa Kinondoni ambaye ni shabiki mkubwa wa Diamond.
zari-na-diamondDiamond na mpenzi wake, Zari
Hili linaweza kutokea pia
Ikazidi kudaiwa kuwa, kuna uwezekano kwa mara ya kwanza Diamond akaamua kuionesha picha ya Nillan bila kuwa na mdhamini au akapata wadhamini lakini akapewa ‘pesa mbuzi’ tofauti na matarajio yake.

Diamond anasemaje?

Kufuatia kumwagika kwa ubuyu huo, paparazi wetu alifanya jitihada za kumtafuta Diamond ambapo alipopatikana alisema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kirefu kwa kuwa bado mazungumzo yanaendelea na anaamini kila kitu kitaenda sawa.

“Kila kitu kinaenda sawa, niliongea na baadhi ya wadhamini na kuwaambia wasubiri mtoto azaliwe, sasa amezaliwa naamini kila kitu kitaenda sawa, hayo mambo ya kubuma siyajui,” alisema Diamond.

Tujikumbushe kidogo

Mwaka jana, Agosti 6, Tiffah alizaliwa na siku chache baadaye akalamba mkataba mnono wa Ubalozi wa Benki ya NMB na maduka makubwa ya vitu vya watoto.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mmmh!Shikamoo Uncle Magu,si hata zile sherehe za kumbukumbu za kuzaliwa zilizokuwa za gharama kubwa mwaka huu zimepungua kwa asilimia 80%,acha tunyooke tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. MAGU KAFANYA WATU TUHESHIANE HAKI MWEEEH.

      Delete
  2. Ndio wanakwenda huko na kujidanganya kuwa wakizaazaaa ama kutotoa vitoto basi watakuwa wameula maviiiiii. Watashangaaaa sana na Serikali hiii. Wawatafute wadhamini huko huko South Africa walipoenda kutotoa hicho kifaranga ama waende wakawatafute hao wadhamini pale Uganda. Na tuone kama watawapata. Watanzania sio wajinga kiasi hicho cha kutoa pesa zao bure na hivi hivi tu eti kisa hicho kifaranga. Kula raha waile akina nani na pesa wazitoe akina nani. Na mshindwe kabisa.

    ReplyDelete
  3. Teh teh teh no kikindo safar hii kiki zimebuma kyumanina...hali ngumu mnoo tunakimbizana na pesa tu..

    ReplyDelete
  4. Tatizo sio pesa tatizo hao wadhamini walipogundua kuwa Diamond atapata mtoto wa kiume ndiyo hapo wadhamini wakakaa pembeni, ilikuwa rahisi kwa Tiffah kupata wadhamini sababu ni mtoto wa kike halafu ndiyo alikuwa mtoto wa kwanza kwa Diamond hivyo ilikuwa rahisi kwa Tiffah, halafu ile 40 ya huyo mtoto wa kiume mbona kimya si walisema itafanyika tarehe 16 mwezi huu ambapo wasanii wengi wakubwa mpaka kutoka Nigeria wangekuja, vipi mbona kimya au na yenyewe imekosa mdhamini?

    ReplyDelete

Top Post Ad