Pata Hii:Mchungaji wa Kilokole Amnajisi Mtoto na Kukimbia Kijiji,Alimchukua Kwao Kwa Ahadi ya Kumsomesha..!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 
MKUU wa Wilaya, Emmanuel Kipole, ameagiza kukamatwa kwa Mtendaji wa Kijiji cha Luchili, Mathias Njolilo na Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Msazibwa Daud kwa tuhuma za kumtorosha Mchungaji wa Kanisa la Agape anayetuhumiwa kunajisi mtoto wa miaka 13 (jina linahifadhiwa).

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake jana, Kipole alisema, haiwezekani Serikali ikemee vitendo vya ukatili kama hivyo huku baadhi ya watumishi wakipokea fedha ili kuficha watuhumiwa.

"Nafuatilia tukio hilo, lakini kama Mtendaji na Mwenyekiti wamemwacha mtuhumiwa,  naagiza vyombo vya usalama viwakamate na wamtafute aliko mtuhumiwa na watoe maelezo kwa nini amemwacha huku akituhumiwa badala ya kumpeleka kwenye vyombo husika," alisema Mkuu wa Wilaya.

Kauli hiyo ya Mkuu wa Wilaya ilikuja baada ya mwandishi wa habari hizi kufuatilia tukio hilo kijijini na kuzungumza na wananchi, huku Mchungaji naye akidaiwa kutoroka kijijini hapo, baada ya kuachwa na viongozi wa kijiji wanaodaiwa kupokea fedha kutoka kwake.

Ilivyokuwa

Mchungaji huyo baada ya kumnajisi moto huyo, alimsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.  

Tukio la kunajisiwa mtoto huyo lilitokea Januari 10 nyumbani kwa Mchungaji huyo lakini licha ya kuomba msaada serikalini ili akamatwe afikishwe kwenye vyombo vya sharia, hakuna hatua zilizochukuliwa.

Licha ya tukio hilo kufikishwa kwenye ofisi ya Serikali ya Kijiji na mtuhumiwa kukamatwa na viongozi hao, aliachwa katika mazingira ya kutatanisha yaliyojenga shaka kwa wananchi, na hajulikani aliko.

Taarifa kutoka kijijini hapo zilieleza kuwa baada ya kufanyiwa ukatili huo motto huyo alitoa taarifa ofisi ya Mtendaji wa Kijiji na mtuhumiwa akakamatwa lakini aliachwa katika mazingira ya kutatanisha.

Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho, Asha Hamud anayeishi jirani na Mchungaji huyo alidai kuwa siku ya tukio mtoto huyo alionekana asubuhi akilia huku akionekana kuvimba mashavu na kutembea kwa shida.

"Nilipomuuliza alisema amefanywa vibaya na Mchungaji usiku kwa kumwingilia  mara tatu na kumsababishia maumivu makali … nilimchukua na kumpeleka ofisi ya Mtendaji wa Kijiji kuomba msaada ili mtuhumiwa akamatwe," alidai mwananchi huyo na kuongeza:

"Baada ya muda Mtendaji wa Kijiji alimtuma Mwenyekiti wa kitongoji cha Luchili Center, Msazibwa Daud ili akamkamate, alimkamata na kumfikisha ofisini hapo na kumfungia kwenye chumba cha mahabusu cha ofisi yake na kusubiri taratibu za kisheria".

Wakiwa wanasubiri taratibu hizo, baada ya nusu saa zilichangwa fedha za nauli ili kumsafirisha mtoto huyo nyumbani kwao mkoani Kagera, ili kupoteza ushahidi wa tukio na kwa taarifa zilizopatikana, aliambiwa anapelekwa hospitalini kumbe alikuwa anasafirishwa.

Mtoto huyo alichukuliwa na Mwenyekiti wa Kijiji, Daudi hadi Sengerema Mjini na kupandishwa basi la Bukoba, huku akiambiwa anapelekwa hospitalini kwa uchunguzi wa afya yake.

Mtoto asimulia 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi akiwa mkoani Kagera mtoto huyo alidai kuwa Mchungaji huyo alimwomba kwa wazazi wake kijijini Izibwa, Bukoba Vijijini kwa lengo la kumsomesha na siku ya nne alipoulizia kuhusu shule Mchungaji alimjibu:  "Shule utakwenda".

Ikiwa ni siku ya nne akiwa nyumbani kwa Mchungaji huyo, alimlazimisha kufanya naye mapenzi huku akimshambulia kwa kipigo.

Dada aeleza

Dada wa mtoto huyo, Devotha Costantine ambaye ni mtoto wa mama yake mdogo, alidai kuwa mdogo wake alifika kwake Kashai mjini Bukoba akiwa na maumivu makali akilalamika kunajisiwa.

"Nilimwuliza kulikoni akasema amenajisiwa na Mchungaji; wakati anamchukua alisema anakwenda kumsomesha, lakini kilichotokea ni kunajisiwa, kitendo ambacho ni cha kikatili, tunaiomba Serikali kumchukulia hatua Mchungaji huyo," alisema Devotha huku akibubujikwa na machozi.

Alisema siku mdogo wake anafika, alishangaa kumwona kwani hakumtarajia.

Kuhusu hali ya mdogo wake, alisema walimpeleka kwenye matibabu na hali yake inaendelea vizuri.

Aidha, mmoja wa wananchi wa Luchili ambaye hakutaka jina lake litajwe gezetini alisema siku moja baada ya tukio hilo, Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji hicho kupitia kwa Mtendaji wake, Mathias Njulilo walituhumiwa kumwacha Mchungaji huyo kwa kupewa Sh 13,000.

Baada ya kumwacha baadhi ya wachungaji wa madhehebu ya kikristo kijijini hapo,  walimchangia nauli akatokomea pasipojulikana na huku wananchi wakitupia lawama uongozi wa kijiji kukumbatia uovu kwa kupewa fedha ili kuficha ukweli na kuomba Serikali iwachukulie hatua kali kisheria.

Mchungaji

Mchungaji anayetuhumiwa kumnajisi mtoto huyo alizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili akisema:

“Namwachia Mungu kwa kuwa ndiye muweza wa yote na yote yanapatika kwa wanadamu, siwezi kusemea lolote juu ya suala hilo limetokea, hata mimi sikutegema naomba msamaha msinitangaze manake ni fedheha kwangu na wachungaji wenzangu aombaye msamaha kama ametenda kosa husamehewa," alisema Mchungaji huyo.

Mtendaji

Mtendaji wa Kijiji, Njolilo alipoulizwa kuhusu kumkamata mtuhumiwa na kumwacha, hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo na kusema hajui lolote licha ya Mwenyekiti wa Kjiji Ibrahimu Mbata kukiri kuwa alipewa Sh 20,000 kama Mwenyekiti wa Kijiji wakiwa ofisini lakini akahoji alipewa za nini na Mtendaji.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad