RAIS Magufuli azuia chakula cha msaada Misenyi.....Awataka Wananchi Wachape Kazi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amezuia serikali kupeleka chakula cha msaada wilayani Misenyi mkoani Kagera kwa madai kuwa wilaya hiyo haina sababu ya kukumbwa na tatizo la njaa.

Rais Magufuli amekataa serikali kupeleka chakula cha msaada katika wilaya hiyo na kusema haikubaliki kwa eneo hilo lenye mvua za kutosha na hali nzuri ya kilimo na kwamba haiwezekani kulia njaa wakati kuna uwezekano wa kuzalisha kwa ajili ya chakula.

Amesema hayo wakati akiweka jiwe la msingi katika kituo cha afya cha kata ya Ishozi Wilayani Misenyi Mkoani Kagera ambapo yupo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo kukagua maendeleo mbalimbali.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli, amesema kuwa serikali haitaweza kujenga makazi ya kila mwathirika wa tetemeko mkoani Kagera kwa kuwa ina jukumu la kujenga miundombinu itakayokuwa na manufaa kwa jamii nzima kama Zahanati, Shule na barabara.

Amesema kuwa kuna baadhi ya watu ambao nyumba zao hazikuharibika kiasi kikubwa lakini wakadanganywa na baadhi ya watu kuwa watajengewa hivyo wakazibomoa kwa kutaka kujengewa nyumba mpya.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. misaada yote hiyo iliyopata kagera kutoka nchi za nje ya mabilioni ya hela bado tu wanataka msaada kutoka serikalini sasa naona hao watu wa kagera wanadeka sana wanataka kila kitu wasaidiwe mpaka chakula ninavyojua ni nyumba tu ndiyo ziliharibika sio chakula, hapo rais kaongea kweli

    ReplyDelete

Top Post Ad