Shehe Mkuu Dar: Diamond Acha Utani na Mungu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

DAR ES SALAAM: Kufuatia kauli ya msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwamba kabla ya kuachia video zake huwa anasali rakaa mbili ndiyo maana huwa zinakubalika kwa watazamaji wake, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum amemjia juu na kumtaka kuacha utani na Mungu.


Kwa kauli yake, wakati akihojiwa na kituo kimoja cha runinga, Diamond alisema huwa anafanya maombi maalum usiku kwa kuswali rakaa mbili kabla ya kuachia video yoyote, jambo alilosema kwamba ndiyo siri ya mafanikio yake.

“Unajua mimi huwa nafanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye video zangu kwa sababu huwa nasali rakaa mbili usiku na kumuomba Mungu ili nifanikiwe kwa video nzuri, nashukuru Mungu anasikia maombi yangu,” alisema Diamond.


Amani lilipomtafuta Shehe Alhadi na kumuuliza kama alichokisema Diamond kina mashiko yoyote kidini, alisema katika dini ya Uislam, muziki wa kidunia ni dhambi na haukubaliki ndiyo maana wasanii kama Mzee Yusuf, wameamua kujiweka nao mbali kwa sababu ni kumkosea Mwenyezi Mungu.

Akaongeza kuwa, alichokisema Diamond ni kama kumfanyia Mungu utani kwa sababu huwezi kuswali, ukamuomba baraka zake ili uende kufanya jambo ambalo ni chukizo mbele zake. Akasema dua za namna hiyo huwa hazipokelewi na Mungu na yeyote anayefanya hivyo, huzidi kumkosea Mungu.

Shehe mwingine aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutochorwa jina gazetini, alisema anachokifanya Diamond ni sawa na mtu ambaye anamuomba Mungu kabla ya kwenda kuiba, jambo ambalo ni tofauti kabisa na misingi ya dini.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mawazo yangu bora mngemuacha tuu Mr chibu

    ReplyDelete
  2. Siku ya kiama utashangaa hata huyo Sheikh anazama motoni. Wanadamu tunamadhambi wote, ila mbaya zaidi badala ya kujitakasa kwanza tuko bize kuyatangaza ya wenzetu kama umeambia Maulana anaomba msaada, upumbavu mtupu. Kila mtut abebe salaba lake mengine mtajuana mbele kwa mbele kwa mbele.

    ReplyDelete
  3. Huyo Sheikh naye ni bomu mzee Yusuph kaamua kuacha mziki ni sawa je mali zote alizopata kutokana na mziki zinaenda wapi? tusiwadanganye wenzetu hakuna binadamu aliyekamilika kila mtu na mapungufu yake. Kweli Diamond anamuomba Mungu na ndo maana anafanikiwa kwani kwa Imani niliyonayo mimi kila kitu kinawezekana kwa uwezo wa Mungu. kama hajapenda huwezi kufanikiwa. Kama kweli mzeee Yusuph kaamua kumrudia Mungu na zile mali zote alizozipata kutoka kwenye mziki kwa vile ulikuwa ni haramu hasiwenazo. Ndo maana kuna sheria kwa watu wanaotakatisha pesa.

    ReplyDelete

Top Post Ad