Ameza Aina Saba za Dawa Ajiue Kisa Shule..!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Milundikwa iliyoko katika Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa mwenye umri wa miaka 15 (jina limehifadhiwa), mkazi wa Kijiji cha Katani, amenusurika kufa baada ya kunywa aina saba za dawa kwa lengo la kujiua akidaiwa hataki shule.

Akizungumza jana eneo la tukio, mama mzazi wa mtoto huyo, Stella Hamis alisema juzi saa 2:00 asubuhi, alimfokea mtoto wake huyo baada ya kumuona nyumbani badala ya kwenda shule.

Stella alisema alimtaka mwanawe aende shule mara moja naye akaelekea shambani.

Hata hivyo, alisema baada ya muda mfupi, mtoto wake huyo alijifungia ndani na kunywa dawa za hospitalini aina saba tofauti zilizokuwapo na kuandaa kamba kwa ajili ya kujinyonga.

"Lakini kwa bahati mmoja wa wana familia, aliingia ndani ya nyumba hiyo na kumkuta mtoto huyo akiwa hajiwezi kutokana na dawa alizokunywa," alisema.

Stella alisema taarifa zilisambaa kwa jirani ambao walifika eneo la tukio la kumchukua mtoto huyo na kumpeleka zahanati ya kijiji kwa matibabu.

Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Solana Kazikodi, alithitibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kazidosi alisema ofisi yake ilipata taarifa mapema juu ya tukio hilo na ndiyo waliofanya kazi ya ziada kuhakikisha mtoto huyo anakimbizwa haraka katika zahanati yao ya kijiji.

Alisema mtoto huyo alifaulu kuendelea na masomo ya sekondari baada ya kufanya vizuri kwenye mtihani wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Katani.

Hata hivyo, alisema tangu aripoti katika shule hiyo, mahudhurio yake yamekuwa ni hafifu kutokana na kutopenda kusoma.

Mganga wa zahanati hiyo, Godfrey Manga, alithibitisha kumpokea mwanafunzi huyo na kwamba alipatiwa matibabu na hakuathiriwa kwa kiwango kikubwa na dawa hizo kwa kuwa walimuwahisha zahanati kupata huduma.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad