AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Simon Sirro amesema Bw. Mbowe aliahidi kwenda mwenyewe juzi tarehe 15, lakini hakwenda lakini jeshi la hilo lilimtafuta usiku na mchana katika makazi yake na kumpigia simu lakini simu yake ilizimwa
Aidha jeshi hilo limesema watuhumiwa watatu Agnes Masogange, Rashid Idd au Chid Mapenzi na Wallis Latif Nasher ambaye ni muuza magari katika eneo la mikocheni watapandishwa kizimbani Jumatatu kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya lakini pia walibainika wanaotumia dawa hizo baada ya kupelekwa kwa Mkemia Mkuu
Katika kupambana na Askari feki, jeshi limemtia mbaroni aliyekuwa askari Magereza wa cheo cha Koplo Peter Elias Msigwa aliyekuwa mtumishi katika gereza la keko, ambaye alifukuzwa kazi Desemba mwaka jana, lakini alikamatwa jana akiwa na mavazi ya kiaskari tena akiwa amejipandisha cheo kutoka koplo hadi Sajenti wa Polisi
Jeshi hilo pia limesema limewatia mbaroni watu 65 kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya pamoja na watuhumiwa 73 wa wizi na ujambazi wa kutumia silaha, mitambo mitano ya Gongo, lita 270 pamoja na Puli 250 za bangi.
Chanzo: Channel Ten
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
nilipokuwa mdogo, nikuwa naitwa kwa jina la utani. lakn sikujali na wal kuanzisha fujo eti kwa sababu ya jina hilo. mwisho likapotea, hata sikumbuki liliishaje!
ReplyDeletemdau hapo juu umeaanisha nn tudadavulie basi ili nasi tujifunze
ReplyDelete