Majibu ya Ommy Dimpoz Baada ya Kudaiwa Kupangishiwa Nyumba na Bilionea

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

DAR ES SALAAM: Madai mazito! Hivi karibuni taarifa imevuja kuwa msanii mkali kwenye gemu la Bongo Fleva ambaye kwa sasa anatamba na ngoma iitwayo Kajiandae kwamba nyumba ‘kali’ anayotamba nayo sasa, amepangiwa na bilioneaa kijana ambaye ni mmoja wa wamiliki wa kampuni moja kubwa jijini.

Habari chengachenga zinaendelea kudai kuwa, mbali na kumpangishia mjengo mkali huyo wa Bongo Fleva, bilionea huyo kijana ndiye kila kitu kwenye maisha yake, anamsapoti kwenye muziki na mambo mengine mengi ikiwemo kumlipia sehemu ya kufanyia mazoezi yaani gym.

Mtoa habari huyo anaendelea kudai, Dimpoz na bilionea huyo wapo karibu sana kiasi kwamba wanawafanya watu kuwa na wasiwasi nao na kama ingekuwa ukaribu wao ni wa mwanaume na mwanamke wangehusishwa kutoka kimapenzi!

“Nakwambieni kweli kuna kitu kinaendelea kati ya Ommy na bosi huyo wa …(anaitaja kampuni), haiwezekani ampangishie nyumba, amlipie gmy na kumsapoti katika kazi zake za muziki. Lazima kuna kitu kinaendelea kati yao,” alisema mtoa habari huyo. UWAZI: Sasa wewe unahisi nini kinaendelea kati yao, si ni washikaji tu?

MTOA HABARI (MH): Hakuna cha ushikaji, ushikaji gani huo, sasa ngoja nikupe siri, mshikaji wake mkubwa na huyo kigogo ni MwanaFA, sasa kwa nini hayupo karibu zaidi ya MwanaFA na yupo na Dimpozi? Huwezi kujiuliza?

UWAZI: Ha Haa haaa! Povu linakutoka sana mzee, kwani hiyo nyumba aliyopangishiwa Dimpoz wewe unajua ipo wapi na analipiwa shilingi ngapi?

MH: Nyie mfanye uchunguzi, wewe unataka kila kitu nikusafishie picha, haya ni hivi, nyumba ipo Mbezi Beach, analipiwa shilingi ngapi, anaishi vipi, kazi kwako na wewe kusafisha picha!

UWAZI: Naona unapaniki mzee, twende taratibu vipi kuhusu hiyo gym anayolipiwa na huyo kigogo, ipo wapi na analipiwa shilingi ngapi?

MH: Aisee una maswali sana, ninachojua gym inaitwa Colosseum halafu siyo Ommy Dimpoz tu, mastaa wengi tu wanafanyia mazoezi pale.

UWAZI: Hao pia wanalipiwa na huyo kigogo?

MH: Sijui kaka, mimi nakupa habari hiyo tu kwa leo (akakata simu).

OMMY DIMPOZI HUYU HAPA

Alipotafutwa Dimpoz kwenye anga zake ili aweze kuanika ukweli kuhusu tuhuma hizo. Dimpoz alipopatikana na kusomewa mashitaka yake ilikuwa hivi;

DIMPOZ: Sasa ndugu yangu hivi ni kila mtu huwa anatafutwa na kuulizwa anapoishi, anaishi vipi, nani anamlipia pango au ni mimi tu?

UWAZI: Aaaa! Watu wanaulizwa hasa mastaa, we eleza ukweli tu mzee.

DIMPOZ: Umesema hiyo nyumba ninayodaiwa kupangiwa ipo wapi?

UWAZI: Eti inasemekana ni Mbezi Beach kaka.

DIMPOZ: Dah! Unaona sasa, mimi naishi kwangu Kigamboni kwa hiyo hayo madai hayana ukweli.

UWAZI: Na unahisi ni kwa nini huo ukaribu wako na huyo kigogo unatiliwa mashaka na watu, na ni kweli kuwa kakulipia gym na anakusapoti kwenye shughuli zako zingine za kimuziki.

DIMPOZI: Kaka naingia benki, siwezi kuzungumza lingine lolote. Dimpozi alikata simu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Manina,kazi kuongeza chumvi kwenye habari.

    ReplyDelete
  2. Mbona nyinyi hamsemi mnaishi wapi?nani anawapangishia nyumba hizo? najua unaweza kupangishiwa na mwanmke hapo inakuwaje? angalia sana mwanamke hana shida sana ila wanaume jiandae na fungus zisizopona tena mdomoni na kinywani, halafu kuzipa njia za mkojo na mwisho tezi dume karibu yako.

    ReplyDelete

Top Post Ad