Zitto Kabwe Afunguka...MANJI Sasa Anaonewa na Kudhalilishwa ili Kumkomoa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Yanayoendelea dhidi ya Yusuf Manji yanashabikiwa na baadhi yetu kwa sababu wanadhani hayatawafika. Tabia ya kukomoa mtu ni tabia mbaya na ina madhara makubwa katika nchi. Ni dhahiri kuwa Manji sasa anaonewa na kudhalilishwa ili kumkomoa kwa sababu ambazo watawala wanazijua wenyewe.

Wakati suala la kutumia unga lipo kortini, Serikali imeamua kumnyanganya hisa zake za Tigo. Sio kwamba Serikali itachukua hisa Hizo, la hasha. Ila Manji azikose tu. Unajiuliza, Serikali hii hii imeacha matapeli wa PAP kuitwaa IPTL na TANESCO inawalipa zaidi ya tshs 300m kila siku. Leo mpaka mahakama inatumia suo moto kurudisha suala la hisa za Manji kwenye Tigo ambalo halina maslahi yeyote ya Taifa. Kwanini Mahakama haikufanya suo moto kurudisha fedha za Tegeta Escrow?

Watanzania wajue tu kuwa, mwaka 2004 Serikali iliachia hisa zake 20% kwenye Tigo kwa USD 750,000 ( vichekesho) kwa kuiuzia kampuni kutoka Luxembourg. Badala ya Serikali kuhangaika na maafisa wake walioachia hisa kutoka nje ya Tanzania wanahangaika na Mtanzania aliyezirudisha hisa Tanzania.

Uhamiaji wanamwita kuhusu wafanyakazi wake wageni kana kwamba yeye Yusuf ni Afisa Rasilimali watu wa kampuni. Aliko Dangote hakuitwa uhamiaji kwa suala la wafanyakazi wake ila Manji anaitwa.

Wakifanikiwa kwa Manji atatafutwa mwengine, Ni sawa na kula nyama ya mtu. Hutaacha.
Manji anaweza kuwa ana madudu mengi Sana, ahukumiwe kwa haki kwa makosa yake. Asikomeshwe kwani ukomeshaji hautaishia kwake. Asionewe. Atendewe haki.
Anyways Kama Mwana Simba, nawasihi Yanga achaneni na mambo ya mabango uwanjani. Hayasaidii lolote.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wapeperushaji wa hii itaviyu ni TBC??

    ReplyDelete
  2. Waache wabebe mabango bana tuone nini kitakacho tokea.........kwa mfano

    ReplyDelete
  3. Mungu hapendi uonevu lakini pia hapendi uovu,kama kweli kuna chuki baina ya Manji na baadhi ya viongozi,au serikali basi amini kuna jambo linakwenda kutokea upande wao,na ndipo ukweli utadhihirika.

    ReplyDelete
  4. Kwa uelewa wangu Manji ni mtu mzima na uenda anajua ni kitu gani kinaendelea, inambidi ajifunze kuwa makini na waliopo madarakani , sasa uenda kukawa na kitu ambacho anakiffanya au alikifanya kwa serikali labda kwa jeuri ya fedha zake, tunasikia pia kumwezesha Edward Lowasa hata baada ya kuhasi chama, hii si sawa yeye ni mwanachama wa chama gani? au ndiyo mamluki? anazo fedha ila pamoja na yote anahitaji kuwa na amani kuliko hata fedha alizonazo. Akubali makosa yake na awaone wahusika na kuomba radhi kwani ukkijua huu wao wanajua ule.Kama ni kujitambua ameishajitambua na kinachofuata ni yeye kuchukuwa hatua stahiki, bado nikjana mdogo na anaweza kufanya mengi zaidi iiwa ataitanguliza busara na hekima badala ya jeuri ya fedha.

    ReplyDelete

Top Post Ad