A - Z ya Paul Makonda Alipokuwa Anaitwa Daudi Albert Bashite Hadi Paul Makonda,Ukweli Huu Hapa..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


1. Alizaliwa tar.15/02/1981 katika kijiji cha Koromije, wilaya ya Misungwi, mkoa wa Mwanza.

2. Majina yake halisi ni Daudi Albert Bashite

3. Alianza darasa la kwanza mwaka 1988 katika shule ya msingi Koromije akitumia majina ya Daudi Albert Bashite. Mwaka 1991 alifeli darasa la 4, akarudia.

4. Mwaka 1992 alifeli tena na hivyo akahamishiwa Mwanza mjini, ili aweze kusoma na kupata masomo ya jioni (tuition).

5. Mwaka 1996 alihitimu darasa la 7 lakini hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya serikali.

6. Mwaka 1997 akajiunga na kidato cha kwanza shule ya sekondari ya Pamba.

7. Mwaka 2000 akahitimu kidato cha 4 na kupata daraja sifuri (division zero).

8. Mwaka 2001 akatumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge (chenye div.3 ya points 25) kujiunga na chuo cha uvuvi Nyegezi (Nyegezi Fisheries Training Institute) kwa masomo ya Certificate akahitimu mwaka 2002.

9. Mwaka huohuo 2002 akitumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge, alijiunga na Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo kwa masomo ya Diploma ya uvuvi (ORDINARY DIPLOMA IN MASTER FISHERMAN, NTA LEV.6), na kuhitimu mwaka 2005.

10. Mwaka 2003 alikutana na Ndg. Benjamin Sitta (mtoto wa Marehemu Samwel Sitta, ambaye ni Meya wa Kinondoni kwa sasa). Wakawa marafiki.

11. Mwaka 2005 baada ya kuhitimu Stashahada yake ya uvuvi, aliomba admission Chuo cha Kilimo Sokoine kusoma shahada lakini akakosa nafasi.

12. Baada ya kukosa nafasi alienda kuishi nyumbani kwa Marehemu Sitta akiwa kama rafiki wa Ben (mtoto wa Sitta). Kwakuwa alitoka familia duni, Sitta aliahidi kumsomesha elimu ya juu.

13. Mwaka 2006, alipata udahili Chuo cha ushirika na biashara Moshi (wakati huo kikiwa chuo kikuu kishiriki cha SUA), kwa kutumia vyeti vyake vya certificate (ya Nyegezi) na diploma (ya Mbegani).

14. Alidahiliwa kwa course ya BA in Cooperate Management & Accounting. Mwaka 2007 alimaliza first year lakini akashindwa kuendelea na 2nd year baada ya kupata Suplementary 6 kati ya Course 8 alizokuwa akisoma (akawa discontinued).

15. Mwaka huohuo 2007 akaomba Admission upya. Akamaliza first year akiwa na carries 3 ambazo alienda nazo 2nd year. Mwaka 2008 akiwa 2nd year akapata supplementary 4 kati ya course 8 alizokua akisoma. Akawa na mzigo wa carry over na supplementary. Akaamua kuacha chuo.

16. Mwaka 2008 akaenda kujaribu kuomba udahili chuo kikuu SUA kwa mara nyingine lakini akakosa.

17. Mwaka 2009 akarudi tena MUCcoBS kwa udahili mpya. Akaachana na CMA akachagua Community & Economic Development (CED).

18. Mwaka 20012 akahitimu shahada ya kwanza ya Community & Economic Development kwa jina la Paul C Makonda badala ya majina yake halisi ya Daudi Albert Bashite

19. Jina Makonda analitumia baada ya kula kiapo mahakamani kubadili jina. Cheti cha Form four kinasomeka Paul C Muyenge lakini vyeti vya elimu ya juu vinasomeka Paul C Makonda baada ya kuapa mahakamani.

20. Ndugu Daudi Albert Bashite ameoa (tangu mwaka 2009) lakini hajabahatika kupata mtoto. Na ndiye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. tufahamu kuwa kila penye nia pana njia,kijana bashite ametisha sio mtu wa kukata tamaa,hii imeonyesha kwamba hakutafuta cheti kwa sababu ya kutafuta kazi bali ni kwa ajili ya kusoma zaidi,amepigana kwa elimu ndio maana akafika hapoalipo.mungu yupo kwa kila anaetafuta kwa bidii.

    ReplyDelete
  2. Jacob Zuma darasa la tatu stop, lakini ni mtawala ktk taifa kubwa kiuchumi barini Africa na raia wa taifa hilo ni wasomikufa mtu ukijumlisha wazungu wenye utajiri mkubwa. Vyeti sio tija ktk uongozi.mradi uwanjani watu na kutii.

    ReplyDelete
  3. Kama anajiamini kweli aache maneno. Tunataka vyeti tuuuuuuuu!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete

Top Post Ad