Agizo la Rais Magufuli Lainyima Usingizi Zanzibar

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wakati Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) likijipanga kuikatia umeme Zanzibar kama alivyoagiza Rais John Magufuli, SMZ inajipanga kuzungumza na shirika hilo ili kuona namna ya kulipa.

Alipotafutwa kwa simu jana kuzungumzia utekelezaji wa agizo hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Dk Tito Mwinuka alisema yupo safarini na hakuzungumza kutokana na mawasiliano kuwa mabaya. 
Baadaye mwandishi wetu alimtumia ujumbe mfupi, lakini Dk Mwinuka hakujibu.

Baada ya kukwama kupata maelezo ya Dk Mwinuka, mwandishi wetu alimtafuta kwa simu, Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji ambaye alisema shirika hilo litatekeleza agizo la Rais kama alivyoagiza. 

“Rais ametoa kauli na kuagiza… lazima tutekeleze,” alisema Muhaji ambaye hakubainisha siku ya kuanza utekelezaji wa agizo hilo.

Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ, Mohamed Aboud Mohamed  alipoulizwa kuhusu deni hilo, alisema wamejiandaa kufanya mazungumzo kati ya mawaziri husika wa pande mbili za Muungano kuona namna wanavyoweza kufanikisha ulipaji wa deni hilo.

“Lengo letu ni kulipa deni lote kwa sababu ukidaiwa lazima ulipe. Tupo tayari kulipa ndiyo maana tumeanza kufanya mazungumzo na wenzetu wa Tanzania Bara, ili kuona namna tunavyoweza kukubaliana juu ya Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco) kulipa hatua kwa hatua ili kumaliza deni lote,” alisema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad