Chirwa Bwana...Soma Hapa Alichokisema Baada ya Kunyoa Upara Danga..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


STRAIKA wa Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa, amebadili mwonekano mpya kichwani kwake baada ya kunyoa nywele zote huku ikielezwa ni kutoa mikosi ili awafunge wapinzani wao Azam FC.

Yanga na Azam zinatarajiwa kukutana kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Mzambia huyo amekuja na staili hiyo huku akiachia ndevu, muonekano ambao ameanza kuonekana nao kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, wakati wa mazoezi ya timu hiyo.

Rafiki wa Chirwa amelsemakuwa Chirwa ameipania mechi dhidi ya Azam, hivyo amepanga kufanya kila jitihada kuhakikisha anawafunga kisha bao atakalofunga liwe zawadi kwa mtoto wake aliyezaliwa wiki iliyopita.

Alipotafutwa Chirwa kuzungumzia hilo alisema:  “Sitaweza kuongea hadi nikapopata ruhusa kutoka kwa kocha.”

Lakini kupitia ukurasa wake wa Instagram alitupia picha yake akiwa mazoezini akiwa na upara na kuandika ‘new look’.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad