Harmorapa Amchana Mose Iyobo Kwenye Interview ‘Nina Hela, Aje Nimwajiri Kama Dancer Wangu’..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Baada ya kuachia track mpya iliyojaa utata utata hivi, Harmorapa ameweka kila kitu ‘clear’ kilichomfanya kuandika mistari ya kumdiss dancer wa Diamond, Mose Iyobo.

Kupitia kipindi cha Fleva Plus kinachoruka hewani kupitia Sunrise Radio, DJ Dix alimuuliza kuhusu chanzo cha kile kinachoendelea kati yake na dancer huyo kutoka WCB.

Harmorapa hakuona noma na alijibu maswali yote aliyoulizwa. Sauti yake iliskika ikisema kwamba Mose Iyobo aambiwe kwamba anahitaji dancer na angetaka awe ni yeye. Aliongeza kuwa anatumia dollars kwahiyo ana uwezo wa kumuajiri na kumlipa vizuri tu.

“Mwambie Mose Iyobo nahitaji dancer, yeah nahitaji dancer kwa sababu naweza mimi, nahitaji dancer so naweza kumlipa kwa sababu Harmorapa ana dollar na pia anatumia account ya dollar,” alisema.

Katika hatua nyingine, alipoulizwa ni kwa nini aliamua kumdiss jamaa kwenye ngoma yake aliyomshirikisha Juma Nature ‘Kiboko Ya Mabishoo’, alisema…”Yani hata mfano naianza ile ngoma nilivyoiandika na nini, mwanzo haikuwa vile ila baada ya kuja kunianza mimi ndo pale nikapata feelings sana nikajikuta naandika vitu ambavyo vinamdiss pia na yeye ili nimjibu.”

Harmorapa anahisi Mose Iyobo alichokoza nyuki pale alipomfananisha na nyani kwa hiyo kung’atwa ni kitu cha lazima. Katika hatua nyingine, rapper huyo alipinga kinachoonekana kama ana nguvu nyingi kwa upande wa ‘publicity stunt’ kuliko muziki wake.

Hali kadhalika, amewataka mashabiki zake wawe tayari kupokea kazi zake kwa kuwa amejipanga vizuri kimuziki mwaka huu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad