Hii Ni Bampa Tu Bampa..Maalim Seif Aagiza Wafuasi Wake Kupambana na Prof Lipumba,Awataka Wasimruhusu Aingize Mguu Wake Zanzibar..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amewataka wafuasi wa chama hicho kulinda ofisi kuu ya Zanzibar dhidi ya uvamizi unaotarajiwa kufanyika.

Akizungumza jana visiwani hapa, Maalim Seif alisema amepata taarifa kuwa Profesa Ibrahim Lipumba na kundi lake wanajiandaa kuvamia makao makuu ya chama hicho Zanzibar.

Alitoa onyo kwa mtu yeyote ambaye atasogea kwenye makao makuu hayo kwa nia ya kufanya fujo, na kuwataka wanachama watiifu wa Zanzibar kuzilinda ofisi hizo.

Aidha, Maalim Seif alimshambulia mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Lipumba kwa kudai kuwavua madaraka wakurugenzi wa CUF Zanzibar na kuteua wakurugenzi wapya.

Akizungumza na wafuasi wake makao makuu ya CUF yaliopo Mtendeni, Maalim Seif alisema Prof. Lipumba hana mamlaka hayo kwani sio mwanachama tena wa chama hicho.

“Kitendo cha Lipumba kuwafukuza wakurugenzi wa CUF Zanzibar na kuwateua wengine, hana uwezo huo kwa sababu yeye si mwanachama," alisema Maalim Seif.

"Na hata angekuwa mwenyekiti halali, (bado) hana uwezo huo kwani wakurugenzi huthibitishwa na baraza kuu la taifa.”

“Vijana nawaambieni suala la kulinda ofisi hii ambayo ni makao makuu pamoja na ofisi ya wilaya iliyopo Kilimahewa Zanzibar sio kazi ya walinzi pekee," alisema Maalim Seif.

"Kila mwanachama azilinde ofisi ili Lipumba na watu wake wasisogee.”

Aidha, kiongozi huyo mkongwe kisiasa alimtaka Lipumba kutoshindana na yeye kwani hawalingani.

Alisema yeye amekuwa na mvuto mkubwa kwa wana CUF na ndiyo maana kila chaguzi amekuwa akipata kura nyingi tofauti na yeye.

Alisema Wazanzibar wana hamu ya serikali ya Zanzibar kuongozwa na CUF hivyo aliwataka wafuasi wa CUF kutowapa nafasi wasaliti wa chama hicho kukivuruga chama.

SALAM ZIMFIKIE

Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amemlaumu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja kwa kuandaa jeshi lake kupambana naye akiwa katika ziara za kichama katika mkoa huo.

“Salamu zimfikie Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja," alisema Maalim Seif. "Na aandae tu hayo mabomu na mimi ziara yangu nitafanya."

"Hakuna wa kunizuia wakati mimi ndiyo katibu mkuu wa CUF ambae nawatembelea wanachama wangu.”

Akizungumza na Nipashe, Kamanda Juma Sadi alimtaka Maalim Seif kupeleka ushahidi wa tuhuma alizotupa dhidi yake.

“Hayo maneno kapewa na nani? Na kama kapewa na wafuasi wake basi wanamdanganya, mimi sijaapa kusema maneno hayo aliyoyadai Maalim Seif dhidi yangu,”alisema Kamanda Sadi.

Kamanda huyo alifafanua kuwa mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa imepigwa marufuku Tanzania nzima, lakini vikao vya ndani hakuna katazo hilo ilimradi havivunji sheria za nchi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Naiangalia serikali hii ya awamu ya tano naona ina dhamira ovu ya kuua upinzani na kuwabagua wananchi kwa itikadi za kichama. Huu mgogoro wa CUF kama serikali inajitathmini na inaelewa muktadha wake basi na iuache ili mahakama za haki zitende haki na Profesa Lipumba ambaye analazimia uenyekiti akae pembeni ili wana CUF waijenge CUF yao na waimarishe upinzani. Sioni kwa jeuri ipi Lipumba anapata ya kutaka kuvamia afisi za CUF visiwani bali naona lengo lake kuu ni kudhoofisha juhudi za CUF kudai haki yao iliyoporwa.

    ReplyDelete
  2. kweli hii ni bampa to bampa maalim seif huachi

    ReplyDelete

Top Post Ad