Jitihada za RC Makonda Zimeuleta Uwanja Huu wa Soka ..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Bila shaka kila mmoja wetu anakumbuka ahadi ya RC Makonda aliyoitoa mwaka jana ya kujenga viwanja vitatu (3) vya mpira kwa ajili ya maendeleo ya mashindano mbalimbali ya michezo ikiwemo Ndondo Cup kwani mashindano haya kwa ujumla wake yanalenga kuboresha mazingira ya michezo na kuzalisha vipaji vingi zaidi ambavyo vinabeba ajira nyingi za vijana ndani yake.

Kimsingi RC Makonda hakuishia tu kuahidi bali alikwenda mbali zaidi na kumualika Balozi wa China nchini Tanzania, Dr. Lu Youqing kushuhudia hali halisi ya viwanja vinavyotumika kwa sasa kama sehemu ushahidi wa kile alichokuwa amemueleza wakati akimshawishi.

Ikiwa imepita miezi kadhaa tangu Balozi kukubaliana na ombi la Mkuu wa Mkoa, jana Machi 3, 2017 Balozi huyo wa China akiwa na RC Makonda wameweka historia mpya baada ya kuweka jiwe la msingi la kuanza ujenzi wa viwanja hivyo, huku wakianza na kiwanja cha Bandari ambacho kitagharimu Dola za Kimarekani 450,000, huku kikijengwa kwa viwango vya kimataifa na kampuni iliyojenga uwanja wetu wa taifa.

Kuonyesha kutambua utendaji na msukumo mkubwa wa RC Makonda katika kutimiza azma ya Rais John Pombe Magufuli ya kutatua changamoto za wanyonge, Balozi pia amemuahidi Mkuu wa Mkoa kufanya yafuatayo:

1. Kuwapatia kipaumbele cha ajira vijana wote watakaoshiriki mashindano ya Ndondo Cup kwenye kampuni mbili za nchi hiyo ambazo zinatarajia kuanza shughuli zake hivi karibuni huku wakitarajia kuajiri zaidi ya vijana 24,000

2. Kuipeleka nchini China timu itakayoshinda michuano hiyo ili ikacheze mechi za kirafiki kama sehemu ya kuwaongezea ujuzi wa soka.

3. Kama haitoshi, timu ya pili na ya tatu kwenye mashindano zitapewa mualiko rasmi kwenye ubalozi wa nchi hiyo.

Kwa namna ya kipekee RC Makonda amemshukuru Balozi huyo kwa kuwa sehemu ya watu ambao wamechangia maendeleo ya jiji la Dar es Salaam na hivyo shughuli za maendeleo ambazo hazikuwepo kwenye bajeti ya serikali kuweza kufanyika pia.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hapa kunachukuliwa faida.mkuu wa mkoa kama alivyosema, alikuwa karibu na ndugu Kikwete. Ndugu kikwete yupo karibu sana na China. Inakuwa rahisi kupitia Mchina kutimiza matakwa mengi sana kwao hata kwa Ridhiwani.lakini si sawa kwa mikoa mingine bila kupata hizi hufuma sababu ni watanzania. Viwanda vingi vimesainiwa na hawa viongozi kwenye maeneo yao. Je kwa mikoa mingine je.wasio na ukaribu na viongozi hawa na Wachina mojakwa moja. Ni hela za watanzania na si pwani na Dar es salaam tu. Viongozi wa nchi ns wa serikali ieangalieni hii.Na wananchi walipakodi inabidi pia tujiulize upendeleo kama huu.

    ReplyDelete

Top Post Ad