Kimenukaa Clouds Media..Mfanyakazi Asimamishwa Clouds kwa Kutangaza Habari ya Paul Makonda, TEF Yaitaka Mitandao Iunge Mkono..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Bodi ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) imekutana jijini Dar es Salaam leo Machi 30, 2017. Pamoja na mambo mengine imejadili mwenendo wa vyombo vya habari ndani ya wiki moja tangu tulipotoa msimamo wa kutotangaza habari za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Bodi imepitia habari za Mkuu wa Mkoa zilizochapishwa tangu ulipotolewa msimamo wa kumfungia. Bodi inapenda kawapongeza wahariri wote waliotekeleza kwa usahihi msimamo wa kutochapisha habari za Mkuu wa Mkoa kwa wiki nzima.

Bodi inapenda kusisitiza kuwa wahariri katika vyombo vya habari; magazeti, radio na televisheni waendelee na msimamo wa kususia habari za Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, hadi atakapotimiza takwa la kuomba radhi kwa tukio la kuvamia kituo cha Clouds.

Bodi inatoa wito kwa viongozi wa mitandao ya kijamii kuunga msimamo huu. Bodi inapenda kufafanua kuwa Mhe. Makonda amewekewa vikwazo Maalum (Smart Sanction) kwa mikutano atakayoiandaa au matukio atakayoyaongoza habari zake hatutazichapisha.

Bodi inakipongeza Kituo cha Clouds kwa kumsimamisha kazi mtangazaji aliyekiuka msimamo wa kutotangaza habari za Makonda. Bodi pia imewasiliana na Uongozi wa UTPC na kukubaliana kwamba msimamo huu uendelee.

Theophil Makunga,
Mwenyekiti TEF
Imetolewa Leo,
Machi 30, 2017
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nyie tu na roho zenu.......hahahaha! Nawaona kama Mnakonda kwa habari za Makonda, na wala sio Makonda kukonda kwa habari zenu........bado yupo yupo sana, na ataendelea kuwepo........japo hamuandiki habari zake, cha ajabu bado mnafuatilia tehetehe..MAKEI NDIO HABARI YA TOWN!

    ReplyDelete
  2. Kama kweli Clouds wamemsimamisha kazi wamemuonea bure, ukweli unabaki pale pale kwamba Makonda ndiye aliyetafuta mfadhili wa kujenga ule uwanja na ndio msimamizi na mfuatiliaji.....wasilete unafiki wao hapa, basi watangaze kukataa ufadhili na usimamizi wa Makonda pia, ili Makonda aondoe wafadhili alowatafuta yeye, Clouds waumalizie wenyewe au watafute mfadhili mwingene kuumalizia, au ndio kusema BANIANI-MBAYA-KIATU-CHAKE-DAWA?? NA HAOMBWI-MTU-RADHI-HAPA

    ReplyDelete
  3. AFADHALI MLIVYOACHA KUMUANDIKA, ANGALAU MTOTO WA WATU ANAPUMUA VIZURI KHAA MLIZIDI WAJAMENI

    ReplyDelete
  4. Bila Za makonda wiki hii mmekula hasara sana.

    ReplyDelete
  5. Kakosa nini KIjana wa watu kubwa mno hata mmemkaa kooni yeye anajaribu kuusaidia UMMA wa WA TANZANIA haswa vijana waliodhirika na matumizi ya madawa ya kulevya na wale wauzaji wakubwa YAANI mmegeza kibao aonekane OVYO je zile FAMILIA zilizo adhirika na watoto pia wadai cheti chake?MUNGU ATAWALLAANI WALE WANAFIKI WAZADIKI WAONGO FITNA NA MAHASIDI kwa kuvalia junga mambo msio yajua NENDENI shule mkaone watu wanaoadhirika na madawa kwa sasa HAKUNA anayesema lolote KIMYA kweli hela inasema watu wamenyamazishwa na hela za HARAMU uzuri wote umegeuka ubaya ya RABII msimamie huyu kijana WAKO

    ReplyDelete
  6. Kuna mambo katika Nchi hutakiwi kushabikia hata kidogo,ushabiki wa uvunjifu amani,kumvunjia heshima Rais na hadhi yake na hata kushawishiwa kumtusi ama kumnunia bosi wako ama mwajiri wako.Media ama mwana habari ni mhimili wa pili wa imani kwa kila Nchi niwaeleze ndugu zangu,Ni kweli mnaungana kumsusia Makonda ama mteule wake Rais, kazi ambazo kimsingi yeye ni mkaazi wa mkoa unaoongozwa na Makonda,Tunasahau Makonda kwa mujibu wa Sheria ndie mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na ndie msimamizi wa shughuli zote za kila siku za Mkoa,tunasahau kazi zetu za kila siku ziko mikononi mwa watendaji wa mkoa akiwemo Makonda,ziara za maendeleo ya mkoa wageni katika Nchi na shughuli za kijamii zina mhusu moja kwa moja kiongozi huyu,hili nilikitanzi la kijinga kabisa,wanahabari mnajivika hivi yakitokea maafa muda huu nani anawajibu kimkoa kutoa tamko?kwa namna moja ama nyingine wanahabari hawasusii habari za Makonda wanasusia kuwahabarisha wana DAR habari za maendeleo kama si matukio ya Dar na Nchi nzima kwa kifupi bila kificho wanasusia habari za Rais wa jamhuri ya muungano na mteule wake na hapa mlengwa si Makonda tena ni Serikali ya JPM,angalizo tu Clouds mmeingia katika vita mbaya mno na mhimili wa dola kwa kuhamasisha haya yanayoendelea mnajua fika Makonda alikuwa nanyi sikuzote kwa nini? mnajua vyema kwanini aliwatembelea usiku ule mnajua vema?Mnajua mipango yote ya mandalizi hadi kutuma kikosi kumhoji mama yule?Mnajua mlivyotumia mbinu na ushawishi mkubwa kuuaminisha umma juu ya kile mlicho kiratibu sawia, Mnafahamu madhara mliyomwingiza kijana mwenzetu NAPE akamwacha Rais Ubungo na Mgeni kutoka Bank ya Dunia mnajua madhara ya footage ile na yule alielekezwa kuirusha ikiwaonyesha askali wale na Makonda?Mnajua kila kitu,Mmeanza na mnaenda ukingoni tegemeeni yafuatayo kutoka serikalini ambapo huyo Makonda wenu anao huo ubavu kwani mko ndani ya mkoa anaouongoza,Tegemeeni kuhojiwa juu ya mialiko ya wanamuziki wenye sifa zile zile Marekani na mienendo ya matamasha yenu na vitendo vinavyotokeaga, tegemeeni serikali ya mkoa kuwadai mapato ya matangazo na viingilio vya matamasha yenu tangu mmeanza,tegemeeni askali wale kurudi kazini kimya kimya wakichunguza tabia za kila mmoja.Kaka Luge yaliyotokea Rwanda na Kenya yalianza namna hii kutoka katika chombo cha habari na wanahabari,Usije ukaambiwa chombo chako ni tishio kwa usalama wa Taifa hili kwa kuchochea chuki,kumbuka bado una BF kubwa na wasanii Nguli na malalamiko ya chini kwa chini dhidi ya maslahi yao juu yenu.KUVAMIWA KWENU KAMA MLIVYOKUITA KUNA MENGI NA YAJAYO YATAOGOPESHA WENGI MSIONE SERIKALI IMEKAA KIMYA WANAJUA KILA HATUA WANAYOKANYAGA NA MAKONDA NI KIJANA TU KIONGOZI ALIYEAMUA KUJILIPUA NA MNAJUA. Kunahaja ya kujipima nini media inakusudia kwa sababu bila ninyi kujua kunafaida kubwa kwa serikali Makonda kuto andikwa andikwa az longer hamuuingilii utendaji wake serikalini atachapa kazi na mwisho media itajikuta agenda aliekuwa anaiendesha kwa maslahi yepi nae ameingia mzima mzima katika mtego huu kumbukeni sababu za hayo yote je ni kweli nguvu hii ni kwasababu aliingia na askali Clouds ama Nyuma ya pazia ni kidonda ndugu cha hasira kali dhidi ya wale wale,Waandishi kwa nafasi zenu chunguzeni jirizisheni na mwisho msiburuzwe kwa maslahi ya wengine.Hii ni vita ya marafiki wawili kukinzana taratibu za kuheshimiana kama ilivyojulikana.Siku zijazo hili halitakuwa la ushabiki ni vita tena sasa ni vita mbaya zaidi BF lenu na Makonda mmelifanya la Kitaifa sasa si Makonda tena ni Serikali ya JPM waungwana wanauliza Mnaandaa mapinduzi?Je mkipewa Pesa na mahasimu wa Serikali katika kampeni yenu na makonda nani ataathirika?Wananchi na serikali yao ama Makonda?yajayo hayaangaliwi Kiurahisi hivyo,hakuna Serikali yoyote Duniani iatakaa kimya juu ya hilli.JIPIMENI CLOUDS NA HICHO KIVULI CHA MAKONDA NYUMA YA KIVULI HICHO YATAIBUKA MENGI DHIDI YA WATU WENU,KAZI ZENU,MARAFIKI ZENU NA MWISHO FAIDA NONO MNAYOPATA KATIKA FULSA MNAZO ANDAA,WAANDISHI TAFAKALI NI MUHIMU SANA

    ReplyDelete
  7. NYIE HIVO MUKOJE HUYU MAKONDA ANABFAIDA GANI KWANZA NI MUONGO PILI KILE ANACHOKIKATAZA YEYE NDIE ANAE ONGOZA KUFANYA KWELI NILIFURAHI ALIVOOANZA KAZI LAKINI ALIKOSEA KUHUSISHA WATU AMBAO WAKO INNOCENT KWANZA JIREKIBISHE MWENYWE HALAFU REKEBISHA UNAOWANGOZA WACHENI KELELE XISIZO KUWA NA MAANA UKWELI UNA BAKI KUWA UKWELI (TOA VYETI KIRI KOSA LAKO,OMBA MSAMAHA KWA ULIO WAKOSEA) WHO THE HELL ARE YOU WEWE NI KAMA BINADAMU YEYOTE ALIUMBWA NA MUNGU SO WACHA KIBURI THEVTRUTH ALWAYS REMAIN THEVTRUTH HATA UFANYE NINI WANAO KUAMINI WEWE NI HAO WASIOONA UKWELI TUNATAKA AMANI BWANA MBONA MUFANO MONGI TUU CHOKO CHOKO ZISIZO KUWA NA MAANA BAADAE UTAVURUGA NCHI WACH KUJIPENDEKEZA KWAVRAISI KWA MASLAHI YAKO BE A MAN

    ReplyDelete

Top Post Ad