Lissu Jeuri Jamani..Eti Amenunua Kesi Ili Akapambane na Serikali Mahakamani..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Baadhi ya wagombea wa nafasi ya  urais kupitia kwa chama cha wanasheria wa Tanganyika TLS wanatarajia kuwasilisha maombi ya kujumuishwa kama wadaiwa katika kesi ya kupinga kufanyika kwa uchaguzi wao uliopangwa kufanyika tarehe 18  ya mwezi huu.

Wamefikia hatua hiyo ili kuuongezea nguvu upande wa wadaiwa kufuatia kesi iliyofunguliwa na wanachama wawili wa chama hicho ambao wamefungua kesi katika mahakama kuu kupitia mkoa wa Dodoma na Dar es salaamu .

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam  mgombea TUNDU LISSU amesema uchaguzi huo umekuwa ukifuatiliwa kwa karibu na watu wengi huku akibainisha kuwa kuna kile alichokiita njama dhidi ya kuuharibu uchaguzi huo

Lissu ameongeza kuwa wanachama wa chama hicho hawatakuwa tayari kuona uchaguzi unasitishwa kutokana na sheria za chama hicho kusisitiza kufanyika kwa uchaguzi wa chama hicho ambacho amedai kimekuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya sheria nchini.

Katika kesi ya msingi ya kupinga uchaguzi huo iliyofunguliwa na wanachama hao, washtakiwa ni mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na chama chenyewe (TLS).

Kwa upande wake mgombea mwingine wa nafasi ya urais ambaye aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani  mheshimiwa LAWRENCE MASHA amebainisha kuwa chama chao hakina kipengele chochote kinachozuia wanasiasa kugombea nafasi ya uongozi katika chama hicho huku akiwataka wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano mkuu wa chama hicho ambao unatarajiwa kufanyika mkaoni Arusha siku ya tarehe 18 ya mwezi huu
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kesi ndio chakula chake,nashauri aachane na ubunge kwa kuwa muda mwingi anashughulikia kesi kuliko kuwa jimboni.

    ReplyDelete

Top Post Ad