Noma Sana..Ridhiwani Atema Cheche kwa Wanaopinga Mama Yake Kuteuliwa Kuwa Mbunge...!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


SIKU moja baada ya Rais John Magufuli kumteua Salma Kikwete ambaye ni mke wa Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete kuwa mbunge, mtoto wake Ridhiwani Kikwete, amepongeza na pia kujibu mapigo ya wale wanaohoji uteuzi huo.


Juzi, taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ilitoa taarifa juu ya uamuzi wa Rais Magufuli kumteua Mama Salma kuwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni sehemu ya nafasi 10 za Rais. Mama Salma ni mbunge wa tisa kuteuliwa ubunge na Rais.

Taarifa ya uteuzi huo iliibua mijadala mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, baadhi wakiunga mkono na wengine wakihoji usahihi wake, huku hoja kuu ikiwa ni upekee wa uteuzi huo ambao ni wa kwanza kumhusisha mke wa Rais mstaafu.

Katika maelezo yake kwa Nipashe jana, Ridhiwani ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze (CCM), alisifu uteuzi huo na kueleza kuwa kadri anavyofahamu, kuteuliwa kwa mama yake kumetokana na jitihada anazozionyesha kila uchao katika kutetea haki za wanawake na usawa wa kijinsia.

Ridhiwani alisema mama yake (Salma) amekuwa akiwawezesha wasichana wengi kupata elimu na pia kusaidia maendeleo ya jamii kwa nguvu kubwa.

Alisema wale wanaohoji uteuzi huo ni haki yao, lakini ukweli unabaki kuwa ni uteuzi sahihi.

“Waliohoji wana haki yao kimtazamo. Lakini la msingi ni kuelewa kuwa Rais amemchagua kutokana na mahitaji ambayo yeye anadhani kuwa Mama Salma anakwenda kusaidia nchi,” alisema Ridhiwani kupitia ufafanuzi wake huo kwa Nipashe na kuongeza:

“Kwangu mimi, nikitaja kazi alizowahi kuzifanya na mafanikio aliyoyapata katika kuhudumia nchi na Watanzania, ninaamini ndiyo sababu za msingi zilizomsukuma Rais kufanya maamuzi (hayo) muhimu na mazuri kipindi hiki.”

Ridhiwani alisisitiza kuwa yeye ni miongoni mwa Watanzania waliofurahishwa na uteuzi huo na kuupokea kwa mikono miwili.

“Nimefurahi kwa uteuzi wake na nimeupokea vizuri. Amekuwa mtetezi wa hazi za wanawake na usawa wa kijinsia … amewawezesha wanawake wengi kupata elimu,” alisema Ridhiwani.

Akieleza zaidi mama yake, Ridhiwani alisema kuteuliwa kwake kutakuwa kumempatia nafasi nzuri ya kupambana ili kurekebisha au kubadilisha changamoto kuwa fursa.

"Wewe ni mwanamke wa Shoka. Hongera sana kwa uteuzi. Imani sasa umepata sehemu ya kuwezesha mapambano kuwa sheria. Mungu akutangulie Mama yangu, Mheshimiwa Mbunge," alisema Ridhiwani kupitia ufafanuzi wake huo.

Mbali ya kuteuliwa kuwa mbunge, Mama Salma pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) ambayo hushughulikia zaidi masuala ya wanawake na usawa wa kijinsia.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndio kashateuliwa hata wakipiga kelele hazisaidiii.

    ReplyDelete
  2. hONGERA mAMA sALMA. hONGERA kIKWETE NA HONGERA TAIFA LETU NA BUNGE LETU TUKUFU..LAZIMA TUWACHANGANYE HAWA WABUNGE ILI WAJITAMBUE HAWA WATORO NA WAKOSA HESHIMA WASIO JIHESHIMU.
    BUNGENI HATUTAKI MAGURUPU NA NINA IMANI MAMA SALMA ANAWEZA KULISAIDIA HILI ILI WAJIELEWE NA KUJUA WAJIBU WAO HAPA BUNGENI NI NINI.. HONGERA NDUGAI..WAMUONA MCHEKULU WA MWAHA YAZAA KUKAYA.. MLUNGU AKUTAZE NA WADODO WOSEEE. MLAMSAJE JEMEDALI MKULU JPJM ... MILIMONYI WAWAHA... HAPA KAZI TU. HONGERA BABA JPJM NA MAJALIWA.. MUNGU IBARIKI NCHI YETU NA WATU WAKE.

    ReplyDelete
  3. hONGERA mAMA sALMA. hONGERA kIKWETE NA HONGERA TAIFA LETU NA BUNGE LETU TUKUFU..LAZIMA TUWACHANGANYE HAWA WABUNGE ILI WAJITAMBUE HAWA WATORO NA WAKOSA HESHIMA WASIO JIHESHIMU.
    BUNGENI HATUTAKI MAGURUPU NA NINA IMANI MAMA SALMA ANAWEZA KULISAIDIA HILI ILI WAJIELEWE NA KUJUA WAJIBU WAO HAPA BUNGENI NI NINI.. HONGERA NDUGAI..WAMUONA MCHEKULU WA MWAHA YAZAA KUKAYA.. MLUNGU AKUTAZE NA WADODO WOSEEE. MLAMSAJE JEMEDALI MKULU JPJM ... MILIMONYI WAWAHA... HAPA KAZI TU. HONGERA BABA JPJM NA MAJALIWA.. MUNGU IBARIKI NCHI YETU NA WATU WAKE.

    ReplyDelete

Top Post Ad