Salma Kikwete Amefuata Nyayo za Hillary Clinton, Graca Machel...!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Uteuzi wa Salma Kikwete kuwa mbunge wa kuteuliwa na Rais umeibua mjadala katika viunga mbalimbali nchini kutokana na ukweli kwamba hilo halikuwahi kutokea katika historia ya Tanzania, lakini kimataifa si jambo geni hata kidogo.

Kwa mara ya kwanza tangu Uhuru, Rais John Magufuli alimteua Mama Salma ambaye ni mke wa Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kuwa mbunge akiwa mteuliwa wa tisa kati ya nafasi 10 za kufanya hivyo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Mama Salma ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, anaungana na wake wengine wa marais duniani kuingia kwenye nafasi za uongozi na siasa.

Hillary Clinton

Mwingine ni Hillary Clinton, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton. Mama huyo ameweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuteuliwa na Demoratic kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni Marekani kabla ya kushindwa kwa Donald Trump, ambaye ni Rais.

Miaka minane iliyopita, Hillary alishindwa na Barack Obama katika mchujo wa kumpata mgombea urais wa chama hicho lakini baada ya Obama kuwa Rais, alimteua kuwa Waziri wa Mambo ya Nje mwanzoni mwa mwaka 2009. Mama huyo pia aliwahi kuwa Seneta wa New York mwaka 2000.

Graça Machel

Katika orodha hiyo pia yumo Graça Machel. Huyu ni mwanamke wa kwanza duniani kuwa ‘first lady’ wa marais wawili tofauti. Alikuwa mke wa Rais wa Msumbiji, Samora Machel kuanzia mwaka 1975 hadi 1986 na mke wa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela tangu 1998 hadi 2013.

Aliteuliwa kuwa waziri wa elimu na utamaduni wa Msumbiji mara baada ya nchi hiyo kupata uhuru na mwaka huohuo akaolewa na Rais Samora.

Winnie Mandela

Aliyewahi kuwa mke wa Rais wa Afrika Kusini, Winnie Mandela ni kati ya wake za marais wanaoingia kwenye historia ya kuwa wanasiasa na viongozi.

Winnie licha ya kushiriki bega kwa bega katika harakati za ukombozi wa nchi hiyo pia amewahi kushika nafasi mbalimbali za kiuongozi serikalini na pia katika chama tawala nchini humo, ANC akiongoza wanawake.

Rosario Murillo

Nchini Nicaragua, Rais Daniel Ortega aliishangaza dunia aliposhinda nafasi hiyo kwa mara ya nne na mkewe aliyekuwa mgombea mwenza kuwa Makamu wa Rais. Rais Ortega alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 72.5 na kuandika historia katika siasa za dunia ya nchi kuongozwa kidemokrasia na mume na mke.

Suala hilo liliipa shida nchi hiyo kujua ataitwa jina gani? Ni First Lady yaani mke wa rais au makamu wa rais.

Janeth Museveni

Miongoni mwao ni Janet Museveni ambaye mumewe, Rais Yoweri Museveni wa Uganda alimteua kuwa waziri wa elimu na michezo katika baraza lake lenye mawaziri na manaibu waziri 80.

Awali, Mama Janeth alikuwa waziri wa masuala ya eneo la Karamoja lililo Kaskazini – Mashariki mwa Uganda ambalo lilikuwa limegubikwa na migogoro na umaskini uliokithiri.

Wasemavyo wachambuzi

Akizungumzia uteuzi wa Mama Salma, Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Benson Bana alisema kuwa mke wa Rais hakumzuii mtu kuteuliwa katika nafasi nyingine ya uongozi ikiwa anazo sifa stahiki.

Alisema hakuna cheo kinachoitwa ‘first lady’ kwenye Katiba na kwamba kilichomfanya ateuliwe ni utendaji wake mzuri aliouonyesha hasa kuguswa na matatizo ya wananchi jambo linalomuongezea sifa ya ziada ya kuwa msemaji wao bungeni.

“Alimsaidia vizuri Rais Kikwete wakati akiwa madarakani. Rais Magufuli amezingatia vigezo, ni haki yake kikatiba,” alisema.

Mratibu wa Taifa wa Taasisi ya wanawake Ulingo, Dk Ave Maria Semakafu alisema, “Amekuwa kwenye siasa muda mrefu sasa, kwahiyo sioni tatizo lolote katika uteuzi huo tunachopigania ni kuongeza nguvu zaidi katika uwakilishi ndani ya Bunge ili kufanikisha hoja za uongozi.”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad