Sasa ni Rasmi Vodacom Tanzania Kuanza Kuuza Hisa Zake Kwa Wawekezaji

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kampuni ya simu za mkononi nchini Vodacom Tanzania itakuwa kampuni ya kwanza inayotoa huduma za mawasiliano kuuza hisa zake katika soko la hisa la Dar es Salaam maarufu kama DSE. Hii inafuatia rasimu ya waraka wa matarajio (Prospectus) na maombi yaliyotumwa kwenye Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kukubaliwa. CMSA ndiyo mamlaka inayosimamia masoko ya mitaji na dhamana nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Ian Ferrao
Uuzaji wa hisa za awali wa Vodacom Tanzania Limited PLC ni katika utekelezaji wa Sheria ya Posta na Mawasiliano iliyofanyiwa marekebisho na sheria ya Fedha mwaka 2016 ambayo inaagiza kampuni zote za simu za mikononi kuuza 25% ya hisa zao kwa umma.
Hisa za kampuni hiyo inayoongoza kwa kuwa na wateja wengi zaidi nchini, huenda sasa zikaanza kuuzwa muda wowote kuanzia wiki hii au wiki ijayo. Vodacom Tanzania inatarajia kuorodhesha asilimia 25 ya hisa zake katika soko la mitaji ambayo ni sawa ni hisa milioni 560 zitakazokuwa na thamani ya shilingi bilioni 476 huku kila hisa ikiuzwa kwa Tsh 850.
Hii ni hatua kubwa sana kwa Vodacom Tanzania ikizingatiwa kwamba kampuni nyingine za simu zinasuasua. Vodacom inatarajiwa kuwa miongoni mwa kampuni zitakazokuwa na mitaji mikubwa katika soko la DSE. Kampuni nyingine zenye mitaji mikubwa ni Acacia, EABL na TBL. Hadi hivi sasa DSE ina kampuni 25 zilizoorodheshwa ambapo kampuni za ndani ni 18 na zile zilizoorodheshwa kutoka masoko ya kigeni yakiwemo London na Nairobi ni 7.
Taarifa rasmi za mauzo ya awali ya hisa hizo milioni 560 lini zitaanza kuuzwa, na wawekezaji gani watakidhi vigezo zitatangazwa hivi karibuni. Tutazidi kukuletea taarifa hizi za uwekezaji kwa makampuni ya simu nchini.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad