Amber Lulu Amgombanisha Young D, Mzazi Mwenzake..Adai Hawezi Kumuacha Young D Ng'ooo..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Ubuyu wa mjini! Video Queen anayefanya poa kwenye Bongo Fleva, Lulu Augen ‘Amber Lulu’, anadaiwa kumgombanisha staa wa Bongo Fleva, David Genzi ‘Young D’ na mzazi mwenzake, Mamisa. Ubuyu huo ulianza pale Mamisa alipoibuka mtandaoni na kummwagia Young D mvua ya matusi yaliyosababisha jamaa huyo kushambuliwa na mashabiki wake.

Mwanaubuyu wetu alilitonya gazeti hili kuwa, chanzo cha matusi yote hayo ni Amber Lulu ambaye anapuliza na kuuma kwani upande mmoja anajifanya hana uhusiano na Young D, lakini wakati mwingine anaonekana naye na wanapendana na kuoneshana mahaba mubashara.

MSIKIE MTOA UBUYU:

“Anayemgombanisha Mamisa na Young D ni Amber Lulu kwani bado ana uhusiano na Young D na wamekuwa wakipika na kupakua ila Amber Lulu akija kwa Mamisa anajifanya wao ni washkaji tu lakini ukweli tunaujua sisi watu wao wa karibu, wale (Young D na Amber Lulu) hawawezi kuachana.”

Mwanaubuyu huo aliendelea kunyetisha kuwa, Amber Lulu amekuwa ‘akimfi cha’ Young D nyumbani kwake, kitendo ambacho kinamsababisha ashindwe kwenda nyumbani kulea familia kwani Mamisa anaishi nyumbani kwa akina Young D na mwanaye aliyezaa na jamaa huyo.

UBUYU WATUA WIKIENDA

Baada ya ubuyu huo kutua kwenye meza ya Wikienda, wanahabari wetu waliuvalia njuga ambapo walianza kwa kumtafuta Mamisa aliyekiri kugombana na Young D na kusema kuwa wanagombana kwa mambo ya kifamilia.

BOFYA HAPA KUMSIKIA MAMISA:

“Ni kweli kumetokea kutoelewa kati yangu na baba mtoto wangu lakini siwezi kuweka wazi mambo ya kifamilia yaliyotokea kwani kwa sasa nimeshamsamehe na namuomba anisamehe kwani ilikuwa ni hasira tu.

“Suala la Amber Lulu, mimi najua ni washkaji tu, mambo ya mapenzi kwao yalishaisha siku nyingi. Anayesema wanaendelea ana nia yake nyingine, mimi nilishawachunguza sana.”

AMBER LULU ANASEMAJE?

Baada ya Mamisa kufunguka, Wikienda lilimtafuta Amber Lulu aliyedai kuwa yeye hawagombanishi wazazi hao bali wanagombana wenyewe na mambo yao. SASA Hata hivyo,

Wikienda lilipoendelea kumbana Amber Lulu juu ya kuwagombanisha wawili hao, mambo yalikuwa hivi;

Wikienda: Amber Lulu kuna madai kuwa wewe ndiye unawagombanisha Mamisa na Young D, je, unalizungumziaje hilo? Kuna ukweli wowote?

Amber Lulu: Kwa nini niwagombanishe? Wao wanagombana wenyewe, mimi hapo ninaingiaje?

Wikienda: Kuna madai kuwa wewe bado una uhusiano na Young D na huwa unakaa naye kwako hadi anashindwa kurudi kulea familia, kwa nini usimuachie mwenzako kwani analea?

Amber Lulu: Siwezi kumuacha Young D, labda yeye aniache mwenyewe, mwambieni aniache ndiyo nitamuacha, hayo mengine siyajui.

NENO LA MHARIRI Ushauri wa Wikienda kwa Mamisa ni kwamba atulie kwanza, amlee mwanaye kwa sababu kama Young D ni fungu lake aliloandikiwa na Mungu, basi atatulia na kuwa mumewe.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad