Dar Yazidi Kuongoza kwa Watoto wa Mitaani..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Serikali imekiri kuwepo kwa ongezeko la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani hasa katika miji mikubwa nchini ambapo takwimu zinaonesha kuwa Jiji la Dar es salaam linaongoza kwa asilimia 28 ya watoto hao nchini

Hayo yamebainishwa leo Bungeni na  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akijibu swali la Mhe Khatib Said Haji Mbunge wa jimbo la Konde aliyetaka kujua serikali inachukua hatua gani kukabiliana na ongezeko la watoto wa mtaani.

"Ni kweli kumekuwa na ongezeko la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani hasa katika miji mikubwa. Kwa mujibu wa takwimu zilizofanyika katika miji ya Dar es Salaam na Mwanza mwaka 2012 zilionesha kuwa Jiji la Dar es Salaam lilikuwa na watoto 5,600 kutoka mikoa 10 ambayo ni Dar es Salaam 28%, Dodoma 8%, Mwanza 7%, Morogoro 7%, Tanga 6%, Iringa 5% Pwani 5%, Kilimanjaro 5% , Arusha 4%". Alisema Waziri Ummy

Aidha Waziri huyo amesema serikali ina jukumu la msingi la kuhakisha ulinzi na usalama kwa watoto hao unapatikana pamoja na kushirikisha jamii iweze kuwasaidia kuwaokoa vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi wakiwemo watoto wa mtaani.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad