AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Manara amesikitishwa na uamuzi uliotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) huku akidai yupo tayari kwa mapambano kwa kuwa hakupewa nafasi ya kusikilizwa.
Haji Manara amesema hayo baada ya kutolewa hukumu na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Jerome Msemwa ya kumfungia kujihusisha na masuala ya soka kutokana na makosa matatu ambayo ni kuituhumu na kuidhalilisha TFF, kueneza chuki za ukabila kwa kudai Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu wake Selestine Mwesigwa kuwa ni Wahaya na viongozi wa zamani wa Yanga na la mwisho kuingilia utendaji wa shirikisho hilo.
Kufuatia maamuzi hayo ya TFF Manara amefunguka haya
"Unazuia na kutonipa nafasi ya kusikilizwa, unanipa hukumu kwa makosa nisiondikiwa katika mashtaka yao..Nipo tayari kwa ajili ya mapambano, tukutane juu". Alisema Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram
Haji Manara amesimamishwa kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja na pia kutakiwa kulipa faini ya Shilingi Milioni tisa.
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
Kuna makosa mengi ndani ya TFF kwa hili swala,lakini pia Simba watakumbana na rungu kama Haji ataamua kuipeleka juu kisheria kwa maana yataongelewa yote na sababu ya TFF kufikia kumfungia Manara.
ReplyDelete