Harmorapa Anusurika Kupondwa Chupa Akiwa Jukwaani..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Usiku wa Jumamosi hii Harmorapa amenusurika kujeruhiwa vibaya na chupa wakati alipokuwa akitumbuiza katika ukumbi wa Maisha Basement uliopo Kijitonyama katika usiku wa Komela.

Akiongea na kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio leo, meneja wa rapper huyo Irene Sabuka amesema, Harmorapa alirushiwa chupa lakini kwa bahati nzuri alikwepa la sivyo yangekuwa yanazungumzwa mengine.

“Kiukweli hili jambo la kusikitisha sana, Harmorapa alikuwa stejini ana perfom ila kabla ya kumaliza show alitokea mtu mmoja akarusha chupa stejini bahati nzuri Harmorapa alikwepa ile chupa. Laiti asingekwepa au ingemkuta kwa bahati mbaya sasa hivi tungekuwa tunazungumza mengine,” amesema meneja huyo.

“Mimi naona kile kitendo ni wivu tu sababu watu hawajui maisha kila mtu ana namna yake anayotokea. Harmorapa ametokea mtaani anatafuta maisha yake leo anaibuka mtu anamrushia chupa na kutaka kumjeruhi, anaibuka mtu mwingine anasema kuwa anataka kumuonesha na kukomesha,” ameongeza.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad