HUKU Wakisema Uchumi Umekuwa..Benki ya Dunia Yainyooshea Kidole Tanzania Kuhusu Madeni..Watoa Kauli Hii kwa Serikali ya JPM..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


WAKATI ripoti ya hali ya uchumi iliyotolewa na Benki ya Duniani (WB) hivi karibuni ikionyesha uchumi wa Tanzania kukua kwa kasi kuliko nchi nyingi Kusini mwa Jangwa la Sahara, Tanzania inaendelea kuwa moja kati ya nchi zenye madeni makubwa miongoni mwa nchi masikini.

Ripoti iliyozinduliwa na WB jijini Dar es Salaam hivi karibuni, inaonyesha uchumi wa Tanzania ukikua kwa asilimia 6-7, wakati ukuaji wa uchumi kwa nchi nyingine zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara ukikuwa kwa asilia moja na nusu.

Pamoja na ukuaji huu mzuri, ripoti hiyo inaonyesha Tanzania kuwa na madeni makubwa, yakichukua asilimia 20 ya pato la ndani.

Hata hivyo, ripoti hiyo inasema, lengo la Serikali kufikia ukuaji wa asilimia 10 kufikia mwaka 2020/21 linaweza kufikiwa kutokana na nchi kuweka msisitizo kuelekea uchumi wa viwanda, pamoja na uwepo wa rasilimali nyingi.

Ripoti hiyo yenye kurasa 88, inaeleza katika ukurasa wa 14 kuwa pamoja na kuwa Deni la Taifa nchi bado inaweza kulimudu, kuna haja ya kuangaliwa kwa umakini mkubwa, kutokana na deni hilo kuongezeka kwa kasi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mlingano kati ta Deni la Taifa na Pato la Ndani (GDP) ulikuwa asilimia 37.7 mwezi Juni 2016,uliongezeka kwa asilimia 2.5 ya GDP ukilinganisha na mwaka 2015.

Ongezeko hilo linaelezewa kusababishwa na ukopaji wa kibiashara kutoka vyanzo vya ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kugharamia miradi ya uwekezaji ya Serikali kutokana na kupungua kwa misaada kutoka nje.

“Kufikia mwezi Juni mwaka 2016, deni la kibiashara lilichukua asilimia 23.3 ya jumla ya deni, huku mikopo isiyo ya muda mrefu na yenye riba nafuu (non-concessional loans), ikichukua asilimia 64.4 ya jumla ya deni la kibiashara.

Pamoja na ongezeko hili, Tanzania bado ipo katika nafasi nzuri ya kumudu deni lake. Hata hivyo, Tanzania inahitaji kuwa makini na deni lake kwa sababu kuna mambo kama kupanda na kushuka kwa gharama za kubadilisha fedha za kigeni, ambazo zinaweza kuwa na athari katika deni,” inasomeka sehemu ya ripoti hiyo.

Akiwasilisha matokea ya ripoti hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Abede Adugna Mchumi kutoka WB, alisema ripoti hiyo inaishauri Tanzania kuwa makini katika ukopaji wake.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hayo ni mahela yaliyokopwa huko nyuma na hao wengine waliopita, manake walikuwa na matumizi ya kujaza mifuko yao wachaaaa,!!!!!! Sasa ndio haya matokeo yake ni madeni

    ReplyDelete

Top Post Ad