Imefichukaa..Huu Hapa Mkakati wa Zitto Kuimaliza Chadema ,Apeleka Hoja kwa Spika Ndugai..!!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Ikiwa ni takribani miaka mitano tangu Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, avurugane na Chadema ambacho kilikuwa chama chake, sasa hali hiyo inaonekana kurudi tena kupitia uchaguzi wa ubunge wa Afrika Mashariki (EALA).

Tofauti na awali ambapo alikosana na Chadema na kufukuzwa uanachama kutokana na kile kilichodaiwa ni kuandaa waraka wa mabadiliko ya 2013, sasa hivi ubunge wa EALA unaonekana kumvuruga tena mwanasiasa huyo na Chadema, baada ya kuandika barua kwa Spika wa Bunge akitaka utaratibu uliotangazwa wa namna ya kupata wabunge ubadilishwe.

Utaratibu huo mpya uliotangazwa, unatoa nafasi kwa wabunge wa EALA kwa mwaka 2017 kulingana na idadi ya wabunge wa kila chama kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Kwa mujibu wa Mwongozo huo, kutokana na idadi ya wabunge wa vyama kwa kila chama, CCM imepata nafasi za wabunge sita kwenda EALA, Chadema mbili, CUF moja, huku ACT Wazalendo  pamoja na NCCR Mageuzi, vikiwa havina nafasi hata moja kwenye Bunge hilo la Afrika Mashariki, kutokana na kuwa na mbunge mmoja kila kimoja, hivyo kutokidhi vigezo.

Kutokana na hali hiyo, Zitto ameliandikia Bunge barua kutaka Kamati ya Kanuni za Bunge ikutane kujadili uchaguzi wa wajumbe wa Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki.

Barua hiyo, ambayo baadhi ya wachambuzi wa siasa wanadai inalenga kutaka utaratibu wa awali ubadilishwe ili chama cha Zitto (ACT Wazalendo), kimwingize mwanachama wake, Profesa Kitila Mkumbo kugombea ubunge huo, inasema mwongozo uliotolewa na Bunge umekwenda kinyume cha Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wanasema endapo hoja ya Zitto ikikubaliwa, ni rahisi zaidi wagombea wa Chadema wakakosa nafasi hizo na badala yake nafasi za upinzani kuiwakilisha Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki zikachukuliwa na wagombea wa ACT na wale wa CUF.

Hali hiyo inaelezwa kuchangiwa na wabunge wengi kwenye Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kuwa ni wa CCM, hivyo ni rahisi kuweka msimamo wa kuwapigia kura wale wagombea wa ACT Wazalendo na wale wa CUF, badala ya wale wa Chadema kutokana na hali ya kisiasa iliyopo nchini kwa sasa.

Barua ya Zitto ya Machi 28 iliyoandikwa kutokana na Tangazo la Bunge kwenye gazeti namba 11 la Machi 17, lililotangaza uchaguzi huo na masharti yake, ilisema mwongozo wa uchaguzi huo unavunja kanuni mbalimbali na kwamba kitakachofanyika sasa kitakuwa ni uteuzi na siyo uchaguzi.

Alisema pia mwongozo huo, mbali na kuvunja Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unataka suala la jinsi lizingatiwe kwenye wabunge wanaokwenda kuiwakilisha nchi katika Bunge hilo.

Baada ya Zitto kuandika malalamiko hayo, Mwanasheria wa Chadema, John Malya, naye aliyajibu akirejea hukumu mbili za kesi ya Anthon Komu (kwenye Divisheni ya Mwanzo na Divisheni ya Rufani).

Malya aliandika kwamba, mwongozo wa Ofisi ya Spika wa Bunge wa kugawa idadi ya viti kwa vyama ni sahihi, kwa sababu Divisheni zote mbili za Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki ziliamua.

Katika sehemu ya barua yake, alisema: “Mwenye kupaswa kubeba mzigo wa makundi ya Zanzibar, Bara na Wanawake (ukiachilia mbali kundi la vyama vya upinzani) ni chama chenye wabunge wengi (CCM)”.

Hoja hiyo ya Malya inachambuliwa na Ado Shaibu, ambaye aliandika ujumbe unaogusa hoja za kisheria ambazo alitumia Malya kukosoa malalamiko ya Zitto.

Shaibu alisema ni kosa kutumia kesi ya Antony Komu ambayo iliamuliwa na Divisheni ya Mwanzo ya Mahakama ya Afrika Mashariki, lakini baadaye Divisheni ya Rufani ya Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki ikatengua hukumu hiyo kwa hoja ya kwamba Divisheni ya Mwanzo ya Mahakama haikuwa na mamlaka ya kuamua suala husika.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad