JB Aungana na Yusuph Mlela Kumporomoshea Lundo la Maneno Nay wa Mitego..Huu Hapa Ujumbe Aliouandika Leo..!!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Ikiwa ni siku moja toka biashara ya filamu ‘feki’ za nje zipigwe marufuku mpaka pale wafanyabiashara wa filamu hizo watakapokamilisha taratibu za ulipaji wa kodi, mengi yameendelea kuibuka, ikiwa ni pamoja na wasanii ambao walihusika kwenye kampeni hiyo kuambiwa wanatumika kisisasa.

Wasanii hao wakiongozwa na JB, Jumatano hii waliungana na ofisi ya Mkoa wa Dar es salaam kufanya opesheni hiyo ndani ya soko la Kariakoo kwa madai filamu hizo zinawanyonya wasanii wa filamu wa ndani kwa kuwa zinauzwa bila kulipiwa kodi wakati wao filamu zao zinalipiwa kodi.

JB amedai amesikitishwa kuona baadhi ya watu wanalihusisha tukio hilo na siasa.

“Ndugu zangu kuna jambo naomba niongee na nyinyi, hivi mnajua tunayoyalilia ni maisha yetu, kwa nini kila kitu mnahusisha na siasa? Hivi ni haki mimi nitozwe 30% ya pato langu mwingine asitozwe?,” aliandika JB Instagram.

“Kwenye shida mimi sitajali nani ananisaidia ilimradi anagusa maslahi yangu, ugali wangu, ninakiri sinema zetu zina mapungufu mengi lakini hiyo siyo sababu za kuacha kudai haki zetu. Ni kama mgonjwa akiumwa leo anapelekwa kwa mganga kesho anapelekwa kuombewa anatetea roho yake. Nawaomba sana hatukatai mkitusema kuwa movie zetu zina matatizo lakini ngoja tumalize hili, tusichanganye, na pia hakuna aliye sema zifungiwe hapana zifate utaratibu kama sisi tunavyo fata. Hizo hizo movie zetu mbovu ndio zinatuwezesha kuishi,” aliongeza.

“Lakini pia lazima mfahamu biashara hii ni kubwa kuliko mnavyodhania, movie 2 zinanitosha kuishi kwa mwaka mzima, ushawaza ni kiasi gani mimi pamoja na kushiriki mapambano haya ni kama nimemaliza muda wangu kwenye kazi hii nimebakiza movie 1 tu. Je udhani mwanao au ndugu yako naye anaweza kuingia huku?. Tukiiponda tasnia huniharibii mimi tu, unaharibu maisha ya watu wengi wajao ambao watafanya vizuri zaidi yetu,” alifafanua zaidi.

Sakata hili limewagawa wasanii wa filamu nchini mara mbili. Wapo ambao wanaamini njia hiyo itasaidia kukuza tasnia ya filamu huku wengine wakipinga njia hiyo kwa madai kua siyo sahihi kwani filamu za nje zilikuwa nchini toka zamani.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Bongo movie kabla hamjaanza kufanya film zenu mulizikuta za nje na mulivoanza kuigiza hata zenu zilikuwa zikinunuliwa sasa iwe muibuke na mandamano yasio kuwa na msingi kizuri cha jiuza hebu kuweni serious sio kutuĺetea film za upuzi halafu nitupe hela yangu kumunua maupuzi yenu wakati kizuri kipo kweli is this right? kweli nyie nuna akiki kwanA kwanini makonda bashite aingiliè why not mwakeyembe kama hataki kiki huyo bashite kufa mbele and why only in movies wakati kuna waimbaji na tuna nunua za nje kama mina lenu basi mutuambie mazirooo musiokuwa na akili think first

    ReplyDelete

Top Post Ad