JIBU la Harmorapa Kuhusu Jinsia Yake Laibua Mshangao Mitandaoni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwanamuziki ambaye amekuja kwa kasi kwenye tasnia ya, Harmorappa au muite Kiboko ya Mabishoo leo amewaacha midomo wazi watu wengi kufuatia jibu lake alilolitoa alipoulizwa kuwa yeye ni mwanaume wa aina gani.

Akiwa katika kipindi cha Kikaangoni kinachorushwa na EATV, Harmorappa aliulizwa swali lililotumwa na shabiki aliyekuwa akifuatilia kipindi hicho ambalo liliuliza, “Wewe ni mwanaume wa aina gani?”  na akijibu swali hilo alisema, “Mimi ni strong woman.” 

Jibu hilo limewashangaza wengi kwa sababu Harmorappa ni mwanaume na hivyo wengi wameshindwa kuelewa kama alielewa swali liliuliza nini au alijibu kama utani.

Alipoulizwa kama anafahamu lugha ya Kiingereza, Harmorappa alisema anaielewa vizuri lakini tatizo ni kwenye kuongea.

“LUGHA YA KIINGEREZA NAIFAHAMU VIZURI LAKINI ILE KUONGEA ONGEA NDIYO SIWEZI” 

Aidha, amesema kuwa kwa sasa hana mpango wa kujiendeleza kimasomo hasa kwenda chuo labda ajifunze zaidi lugha ya Kiingereza. Kuhusu suala la kujiunga WCB, alisema, “Siwezi kujiunga WCB hata kwa shilingi ngapi, Sizuzuki na hela, maana kama ni hela hata mimi mwenyewe ninazo.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad