Kudadeki..Waakenya Nao Waanza Kuisoma Namba,Serikali ya Uhuru Kenyatta Yasitisha Ajira na Kubana Matumizi..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Bajeti ya Kenya ya mwaka 2017/2018, imesomwa jana kinyume na inavyosomwa kawaida mwezi Juni, kutokana na uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka huu, huku ikitangaza kusimamisha ajira katika sekta ya umma.

Katika bajeti hiyo ya shilingi za Kenya trilioni 2.6 (Takriban shilingi trilioni 52 za Tanzania) Waziri wa Fedha, wa nchi hiyo, Henry Rotich ameondoa kodi kwenye mahindi yanayoagizwa kutoka nje kwa kipindi cha miezi minne ijayo,

Aidha kodi imeondolewa kwenye dawa za kuulia wadudu za nchini humo pamoja na magari ya utalii yanayoundwa nchini Kenya.

Katika bajeti hiyo ambayo ni ya mwisho kwa serikali ya Jubilee katika muhula wake wa kwanza, serikali imeongeza kodi kwenye kamari hadi 50% kutoka 7.5% ya awali kama njia ya kukomesha uchezaji kamari.

Serikali pia imetangaza kusimamisha ajira katika sekta za umma isipokuwa sekta ya elimu kama njia ya kupunguza matumizi.

Jumla ya Shilingi bilioni 524.6 za kenya katika bajeti hiyo zitatokana na mikopo kutoka nje na ndani ya nchi.

Shilingi bilioni 2 za Kenya  zimetengwa kuwaajiri walimu, na zingine bilioni 4 kuwalipia mtihani wanafunzi wa darasa la nane na kidato cha nnemwaka 2017 na 2018 huku serikali za kaunti zikipata jumla la shilingi bilioni 329.

Ili kuhakikisha kuwa vijana wana ajira, serikali imetenga shilingi milioni 450 Ksh kwa kuboresha kiwanda cha Rivatex, na zingine milioni 250 kuboresha kiwanda cha maziwa cha New KCC.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad