Kumekucha...! Bifu la Watangazi wa Shilawadu na RC Makonda Lafikia Patamu na Limenoga Sasa..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wakiwa katika Kipindi chao ambacho kilikuwa mubashara kabisa Mtangazaji muongozaji wa Kipindi pendwa na Watanzania wengi hadi Mheshimiwa Rais wetu JPM aitwae Soud Brown amekuwa kila mara akifumba Fumbo huku akicheka mno na mwenzake Kwissa.

Ukiwaangalia zaidi utagundua kuwa kwa yale yaliyowatokea wiki mbili zilizopita utagundua kuwa Kipindi chao Kizima cha leo ni kama vile na wao wameamua kulipiza Kisasi kwa waliyofanyiwa na ' Mvamizi ' Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul Christian Makonda.

Mtangazaji Soud Brown amekuwa kila mara akifumba fumbo moja hilo hilo huku akilinogesha na Kiitikio na Mistari iliyopo katika Wimbo maarufu wa Ney wa Mitego wa WAPO huku kila mara akimuuliza mwenzie kuwa ' Je mlango wetu umefungwa? '.

Fumbo lenyewe la Mtangazaji Soud Brown ambalo si Siri kuwa amelielekeza ' makusudically ' kabisa kwa ' adui ' yao na ' mvamizi ' wao Makonda ni kama lifuatalo nalinukuu " Hata wanaovua Viatu na Soksi zao zinanuka Wapo........unasema Wapo.......hata wanaonuka Midomo pia Wapo......unasema Wapo.....Oya Kwissa umefunga mlango lakini?...... Jamani hata wanaonuka miguu wakivua Viatu vyao Wapo.......unasema Wapo......hata wanaonuka Midomo sana Wapo......unasema Wapo......Kaka angalia umefunga lakini mlango? Walinzi wapo gado?

Sasa Kazi imeanza na naomba mlio karibu na hawa Watangazi akina Soud Brown na Kwissa mtusaidie kutuulizia kutoka Kwao kuwa huyo anayenuka Soksi na Miguu akivua Viatu ni nani? Halafu na huyo anayenuka mdomo pia ni nani?

Chokoza wote lakini kamwe usichokoze na kuanzisha vita na Waandishi wa Habari kwani wana mbinu nyingi za kukuchafua, kukumaliza na ikibidi hata kukudhalilisha. Pole sana ' mvamizi ' Mkuu wa Clouds nadhani sasa Vita baina yako na wao ndiyo imeanza na imefika patamu mno.

Kuna Watu wanajua mno kulipiza Visasi hasa kwa waliyofanyiwa au mateso ya kimanyanyaso waliyopata.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Naona mimi labda akili yangu haina akili, mimi ninachojua kuhusu neno au kitendo cha kuvamia ni kwamba watu wamevamiwa na wameumizwa watu kadhaa au watu kadhaa wameuawa. sasa huu uvamiaji wa RC Makonda ambao watu wamekazana amevamia amevamia na askari wenye silaha za moto jamani mkuu wa Mkoa si ana walinzi wake au inakuwaje mbona mimi sielewi jamani. RC Makonda endelea kukaa kimya tujiulize na tujijibu wenyewe.watanzania tumepoteza mwelekeo baada ya kufanya kazi kutwa kucha kuangalia mambo ambayo hayana msingi wowote tunapotea jamani.MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tafuta definition ya kuvamia utaelewa maana yake na si mpaka uue au ujeruhi. Sina mlengo wowote but nilitaka kukupa tu kazi ndogo

      Delete
  2. Clouds wauza Unga Maarufu hao walisha muuwa Ngwea watu hawajui tu kama wa deal na Chui aliye jivisha Mgozi ya Kondoo!!! Ila ipo siku yao wataumbuka tu....

    ReplyDelete
  3. Definition ya uvamizi bro haitoshi, sasa na wewe jibu swali lifuatalo, Majambazi yamevamia benki ya NBC, dula kubadirishia fedha za kigeni, au kuvamia mashamba ya wakulima inavyo fanywa na wafugaji, hivi wewe inakuja kichwani mtu mmeelewana kufanya jambo fulani na flash mmepeana hapo kabla baadae anafika kuona kama makubaliano yenu yamefikiwa ama laa, wee unabadilisha kibao kuwa amevamia, hivi Rc Makonda alishindwa kuvamia BOT au Stanbic tena akiwa na askari 6 aje kuvamia CLOUDS?, ndiyomaana hata baadji ya watu uteuzi wao umesitishwa kwa kufanya kazi kama remote na kusahau aliyekuajiri, sasa akawaone SOUD BROWN wamaana tena, wao wanafanya kazi tena kwa nafasi yeye inakuwaje sasa? issue ilivyokuwa haikuhitaji uharaka wa namna hiyo bila ya kuwahusisha wenye mamlakaza juu ni kosa kubwa. Je hiyo tume ya uchunguzi ilikuwa fair kwa hali ilivyokuwa? waipata hadidu za rejea za kutosha au zilikuwa ni moja kwa moja kumuona mmoja ndiye mwenye makosa? kwa kifupi tume hiyo ilikuwa batili na time frame ya tume hiyo ya saa 24 haikuwa sawa, tujifunze kusema ukweli na kufanya anaysis vizuri, tusisukumwe na chuki na revenge kwani mwisho wa siku zinakurejea mwenyewe.

    ReplyDelete

Top Post Ad