AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Mshauri wa Rais Donald Trump wa masuala ya usalama, Herbert Raymond McMaster amesema kuwa Marekani na China zinaelekea kupoteza uvumilivu dhidi ya Korea Kaskazini inayoendelea na vitisho vya silaha za Nyuklia.
McMaster amesema makubaliano yanayojitokeza dhidi ya tabia ya vitisho vya Korea Kaskazini kwa sasa yanaijumuisha China.
Amesema kuwa kuna makubaliano ya kimataifa, ikiwemo China kuhakikisha tabia hii haiendelei, kwani kumekuwa na majaribio ya makombora ya hivi karibuni yanayoonyesha tabia ya vitisho ya Korea Kaskazini hali ambayo hawataivumilia zaidi.
Amesema kuwa Rais Trump ameweka wazi kuwa Marekani na washirika wake hawatokubali kuona utawala wa vitisho dhidi ya silaha za nyuklia.
Korea Kaskazini imefanya jaribio la uzinduzi wa makombora ya masafa ya mbali, hata hivyo lilikwama, ambapo Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence amefika Korea Kusini saa chache baada ya jaribio hilo.
Akizungumza katika kambi ya jeshi, Pence amesema anawahakikishia kuwa chini ya uongozi wa Rais Trump ushirika wa Marekani Korea Kusini haujawahi kuwa na nguvu lakini kwa msaada wa jeshi hilo na Mungu uhuru utaendelea kuimarika katika rasi ya Korea bila vitisho vyovyote
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
WAENDE TU KAMA SOMALIA MBONA HADITHI NYINGI
ReplyDelete