MC Algiers Yaja na Nyota 18..Watoa Neno Hii Moja Tu kwa Yanga..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


MC Algiers itawasili leo usiku jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo wake wa kwanza wa kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga.

MC Algiers imesafiri na wachezaji 18 huku ikilazimika kuwaacha majeruhi mabeki Azzi na Boudebouda, ambao wanategemea kurejea katika mechi ya marudiano jijini Algiers.

Kocha Kamel Mouassa ambaye hajashinda katika mechi zake mbili za kwanza alizocheza ugenini dhidi ya Bechem United na FC Renaissance amesema wanataka kufanya mabadiliko suala hilo "Ni ukweli kwamba hatujashinda mechi mbili tulizocheza  Ghana na DR Congo; Siwezi kulificha hilo kwa wakati huu kwenu sababu tumekuwa tukishinda mechi za nyumbani.

"Tunajua haitakuwa kazi nyepesi kushindi ugenini, lakini tutafanya kila kitu kuhakikisha tunashinda nyumban. Kama tukishindwa kuwafunga kwao tunatakiwa kufunga japo bao moja ugenini litatusaidia katika mechi ya marudiano, "alisema Mouassa.

Naye nahodha Hachoud alisema: "Tuna mechi mbili za kutufikisha hatua ya makundi, tunatakiwa kupata matokeo mazuro Dar es Salaam ili kufuzu kwa hatua ya makundi. Hatupaswi kufanya makosa katika mechi hizo mbili, iwe Jumamosi au hapa Algiers. "

Kikosi cha MC Algiers: Chaouchi, Chaal, Hachoud, Karaoui, Bouhenna, Mebarakou, Demou, Kacem,  Chita, Derrardja, Seguer, Aouedj, Bouguèche, Nekkache, Djemaouni , Zerdab, Gourmi.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad