Mwakyembe: Ntahakikisha Nawapata Waliomteka Roma ili Kukomesha Tabia Hii..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesikitishwa na vitendo walivyofanyiwa wasanii wa muziki Roma Mkatoliki na wenzake huku akisema hawezi kukubali kuona mambo kama hayo yakiwa yanaendelea kutokea.

Akizungumza na wanahabari jana Jijini Dar es Salaam, Waziri huyo amesema kilichotokea siyo hali ya kawaida kwa watanzania kamwe hawezi kukubaliana na jambo hilo huku akisisitiza kuwa atafuatilia kwa ukaribu sana ili aweze kupata majibu ya haraka kabla hajawasilisha bajeti ya wizara yake

"Hiki kilichotokea siyo hali ya kawaida kwa watanzania, hatuwezi kukubali kitu kama hiki kiendelee kutokea,nitalifuatilia kwa ukaribu sana, nitajitahidi nipate majibu kabla ya bajeti yangu Bungeni". Alisema Dk. Mwakyembe

Hata hivyo Dkt. Mwakyembe amewataka wananchi waache tabia ya kuamini kila maneno yanayosemwa na watu ambao hawana ujuzi katika masuala ya uchunguzi, hivyo wanapaswa kuvipa muda vyombo vya dola viweze kufanya kazi zake kwa ufasaha.

"Nilishasema kuwa nimeagiza vyombo vya dola vifanye uchunguzi ili ajulikane aliyewafanyia hivi wakina Roma kama ni nani kama wa dola ntadili naye, tuache uchunguzi ufanyike, tuache kupiga ramli". Alisisitiza Mwakyembe

Pia Waziri huyo mwenye dhamana na wasanii ametoa ujumbe kwa vyombo vyote vilivyopo chini ya Wizara yake kutofanya mahojiano yoyote yanayowahusu wasanii hao bila ya kuwepo taarifa kamili kutoka kwake.

Kwa upande mwingine Roma ambaye ambaye amesimulia tukio lilivyokuwa amesema kwa sasa hawezi kuongea mambo mengi kwa kuwa kila kitu amekwisharipoti polisi kila kitu, na kwamba kuna mambo akiyaweka hadharani atakuwa anaingilia upelelezi wa polisi.

Pia amesema hawezi kujua kama kweli tukio hilo lililowatokea  linahusiana na muziki kwa kuwa ameweza kuhusishwa mpaka mfanyakazi wao wa ndani ambaye hana hata chembechembe za uimbaji.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Inaudhi kweli hizo bla bla bla za huyo mkuu kana kwamba hajui what happened wakati anajua fika ni akina nani wanate da hayo maovu na kwa agizo la nani lkn Mungu kamwe huwa halali he's watching all evil works what goes around comes around

    ReplyDelete

Top Post Ad