Mwana FA. - East Coast Team Haitarudi Tena .!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Msanii wa 'HipHop' Bongo Mwana FA amefunguka na kusema kundi la East Coast Team halitaweza kurudi tena katika mambo ya muziki tofauti na taarifa za awali za kurejea upya kwa kundi hilo.

FA ameuweka wazi ukweli huo akiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio kwa  kusema itakuwa vigumu kurudisha kundi hilo tena katika ulingo wa muziki lakini wanachoweza kipindi hiki ni kufanya 'collabo' ambayo itakuwa inawakutanisha pamoja yeye GK na AY.

"Tulifanya ngoma mbili tatu ila hatukukubaliana kuziachia pia East Coast haiwezi kurudi kwa pamoja lakini mimi, GK na AY tunaweza kufanya kazi kwa pamoja kwani ni jambo rahisi". Alisema FA

Pamoja na hayo msanii huyo amesema tayari amesharekodi kazi nyingi amezihifadhi maktaba kwake kwa kuwa anaogopa kuzitoa katika kipindi hiki.

Nina kazi nyingi katika maktaba nasubiria 'timing' tu niachie maana sasa hivi kuna mambo mengi yanaendelea unaweza ukatoa wimbo hamna mtu anayesikiliza, watu wanaweka bando kufuatilia ubuyu tu, kwahiyo acha patulie kidogo tutaangusha" Alisema FA

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad